El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 297
- 537
Wiki hii kwangu imenipa kufikiri sana. Mitandao ya kijamii na habari iliyozagaa sana huko, ilikuwa kuhusu usafiri wa mabasi ambao viongozi, wakuu wa nchi waliotumia kwenye mazishi ya malkia wa uingereza.
Ukiacha masuala ya kiufundi kama ya kiprotokali na ulinzi (ambayo nina hakika hao waliofanya hivyo wanajua, kumbuka hao ni waingereza au Sema first class world), Kuna Sababu gani ya kushangaa viongozi kupanda mabasi?
Hapo ndo inafika mahali pa kujua hasa kwamba Sisi Africa na hasa Tanzania, tunawaza kidogo (trivially) na tunawafanya viongozi miungu watu.
Kwa nini ushangae kiongozi kutumia usafiri wa basi? Je yeye siyo mtu kama ulivyo wewe unayetumia usafiri huo na uliyemfanya kuwa kiongozi?
Huyo kiongozi katoka sayari gani ambayo sisi hatuikai?
Je, akipanda basi hatafika mahali yalipo matanga? Mahali ambapo ni karibu tu.
Ni vizuri sawa kuwapenda viongozi, lakini iwe kwa kiasi na inapositahili. Kwa sababu nje ya hapo viongozi hawa watageuka kuwa miungu watu na badala ya kuwa watumishi wetu, tutageuka na kuanza kuwaabudu.
Kusifia viongozi kulikozidi, kutowahoji au kuonyesha kutoridhika na huduma Yao kwetu, kuwatetea kutumia private presidential escort Mahali kama uingereza hizo ni dalili siyo tu za kuwa na mawazo madogo (small thinking) bali ni kibali cha kuwafanya viongozi kutudharau na kutowajibika kwetu Kwa mambo ya msingi yanayotuhusu.
Viongozi huitengeneza jamii Kwa mambo fulani, lakini jamii nayo huwatengeneza viongozi inaowataka.
Jamii ya kuabudu viongozi, isiyowaona viongozi kwamba ni watumishi wao na kwamba wao ndo wamewafanya kuwa viongozi. Jamii isiyouliza viongozi wao maswali magumu, jamii isiyopinga (protest) mambo mabaya ambayo viongozi wanayafanya, hii itakuwa jamii ambayo siyo tu viongozi hao wataidharau, bali hawatawajika inavyopaswa Kwa jamii hiyo.
Jamii ambayo mpaka umsifie Rais, ndo uanze kuongea hata mahali ambapo Rais hayupo, jamii inayotetea Rais kutopanda basi badala ya kumdai maendeleo, inaazaa viongozi wasiowajibika kabisa kwa wananchi wao.
It is not only a leader who shapes a society. The society also shapes it's leader in a required manner.
Napenda kuona jamii inayoheshimu viongozi na siyo kuwaabudu kama ninavyoona, jamii inayofikiri mambo makubwa ya kimaendeleo na siyo kutetea umaarufu wa viongozi kila siku kama kwamba wao si watu bali miungu.
Africa Ina ugonjwa huo wa kushabikia viongozi (sycophancy). Na ndo maana huoni wazungu wanaongea juu ya usafiri wa mabasi Kwa viongozi, which is so trivial Bali utawaona wakipiga kelele wanapoona hakuna kile unachoongoza kwacho (service delivery)
Let's stop being sycophants of Leaders let's make them accountable.