Afrika: Watu milioni 239 wakabiliwa na njaa na utapiamlo

Afrika: Watu milioni 239 wakabiliwa na njaa na utapiamlo

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa FAO Marina Helena Semedo amesema takriban watu milioni 239 wa Kusini mwa Jangwa la Sahara wanakabiliwa na tatizo la njaa na utapiamlo.

Amesema njia pekee ya kutokomeza masaibu hayo ni kupitia amani na usalama wa kudumu barani Afrika. FAO hivi sasa inatekeleza shughuli mbalimbali za kuongeza mapato kwa ajili ya watu wa vijijini walio masikini.

Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa yameweka malengo kadhaa muhimu ikiwemo ya kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya Waafrika wanaoishi katika hali ya umasikini, njaa, na utapiamlo, kwa kuwawezesha kwenye kilimo ili kusukuma mbele juhudi za nchi kufikia ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030.

Kamishna wa Kilimo katika Umoja wa Afrika Josefa Sacko amesema kuna haja ya kuwasilishwa mbinu mpya za kukabiliana na changamoto za njaa na umasikini barani Afrika.

Amesema wakati umefika kukiri kuwa mbinu zinazotumika sasa haziwezi kuzaa matunda. Kumaliza migogoro Afrika ni muhimu kutatua matatizo ya chakula.

Chanzo: ParsToday Kiswahili
 
Back
Top Bottom