Afrika yagundua gari la umeme la bila kuchaji Marekani wagoma kulisajili halifwati kanuni za physics

Afrika yagundua gari la umeme la bila kuchaji Marekani wagoma kulisajili halifwati kanuni za physics

Marekani wasajili kwani wameambiwa gari inauzwa Marekani?

Kama gari inauzwa nchini kwake na Africa inatosha wawapuuze Europeans kamwe Europeans hawatalikubali sababu itaua biashara zao
South Africa wanatengeneza magari ya kijeshi wanauza Marekani. Morocco wanaunda magari wanauza Ufaransa na Spain.

Nyinyi mpo hapa mnajiliza eti Mzimbabwe kakatazwa kibali cha kuunda gari na Marekani. Toyota, Suzuki, Honda, Volkwagen, Hyundai, BYD, GWM, Mitsubishi na makampuni chungu nzima duniani huwa yanalazimika kuomba ruhusa Marekani???

Kwa mtu anayejua Physics kidogo na economics kidogo anajua kabisa hizo porojo za Mzimbabwe ni pumba tu za kudanganya wehu.
 
Sijaona shida yeyote hapo ye atengeneze aanze na piki piki za mawimbi ya radio kwanza bei MILION 2 atuuzie sis hatutaki mambo ya physics Wala nn ili mradi chuma itembee moto moto tusombee matofali, Nguruwe tubebe na ma pic YESU NA MARIA mwambie anachelewa
 
Nmekumbuka kile kisa cha jamaa kwenye ugomvi anakimbilia kusema ''nishikeni au nitampiga vibaya sana''. Au kile cha raia mmoja huko Zenji ''alivumbua'' helkopta lakini akawa anasema serikali inamnyima vibali. Waafrika sisi kelele na kulalamika ndiyo uvumbuzi wetu. Hii habari inaonyesha hakuna ugunduzi wowote bali ni maneno matupu. Kama ameweza kufanya maajabu kama hayo anataka vibali vya wazungu vya nini? Si auze magari yake huko Zimbabwe na nchi nyingine za Afrika? Habari kama hizi huwa zinasikika sana Afrika ili kuondoa inferiority complex tuliyonayo ya ku-fail kwa kila jambo.
Ndo yale ya dawa za asili eti mzungu kawanyima kibali inferiority complex.
Kama unatibu ukimwi,kansa si utibu tu uponye watu watakutangaza wenyewe
 
Kuthibisha tecnolojia yake maana yake ni Kutoa Siri za hiyo tecnolojia yake
Akisha toa hiyo Siri mawili eidha aibiwe huo ujuzi au waangalie jinsi ya kudhibiti huo ujuzi

Mbona wao zana zao za kivita wanaficha tecnolojia yake?

Uthibitisho pekee ni kuliwasha na kutembea nalo wiki 2 au 3 bila ya kulizima

Hawa Wazungu wanapenda sana kuturudisha nyuma
Awashe Sasa
 
South Africa wanatengeneza magari ya kijeshi wanauza Marekani. Morocco wanaunda magari wanauza Ufaransa na Spain.

Nyinyi mpo hapa mnajiliza eti Mzimbabwe kakatazwa kibali cha kuunda gari na Marekani. Toyota, Suzuki, Honda, Volkwagen, Hyundai, BYD, GWM, Mitsubishi na makampuni chungu nzima duniani huwa yanalazimika kuomba ruhusa Marekani???

Kwa mtu anayejua Physics kidogo na economics kidogo anajua kabisa hizo porojo za Mzimbabwe ni pumba tu za kudanganya wehu.
Huyu jamaa ni muongo, mdanganyifu na tapeli kwa kiwango Abdul Samiah.
 
Huu ni uongo. Kuwa gari linatakiwa kusajiliwa marekani ndo litumike? Ujinga. Atengeneze mengi auze. Rahisi tu wala hamna haja ya kubabaisha babaisha. Atauza tu. Alikatie Haki/Hati Miliki. Hahitaji wamarekani wa li pitishe.
 
Hakuna kitu hapa. Ni wajinga wachache wana-share propaganda za kujiliwaza tu ili ionekane kama mwafrika anaonewa. Kwanza habari yenye haingii akilini kwa mtu mwenye kuijua dunia. Hivi ukigundua kitu kama hicho utaomba ''vibali'' kutoka kwa wazungu? Si unatengeneza magari yako na kuyauza hata nchini kwako?
Waafrika wajinga sana.
 
Yaweza kuwa uongo ila nadhani kama ni ukweli shetani hatakubali.
 
Mvumbuzi wa Zimbabwe Awasilisha Gari la Umeme Linalojiendesha Bila Kuchaji: Mapinduzi Katika Teknolojia ya Magari

Mvumbuzi wa Zimbabwe, Maxwell Chikumbutso, ameunda gari la kwanza la umeme duniani linalojiendesha kwa radio wave energy technology, likivunja kanuni za kawaida za magari ya umeme.

Maxwell Chikumbutso, mvumbuzi kutoka Saith Group, amewasilisha uvumbuzi wa kipekee katika sekta ya magari ya umeme (Electric Vehicles - EVs)—gari linalojiendesha bila kuhitaji kuchajiwa kutoka chanzo cha nje.

Katika maonyesho yaliyofanyika State House, Harare, Chikumbutso alimwonyesha Rais Emmerson Mnangagwa teknolojia hii, akieleza jinsi gari hilo linavyotumia radio waves kuzalisha nishati yake yenyewe. Teknolojia hii inatoa matumaini makubwa kwa sekta ya usafiri na nishati, huku ikiibua maswali kuhusu uhalisia wake katika ulimwengu wa kisayansi.

Faida Muhimu za Teknolojia Hii

Hakuna haja ya kuchaji gari – Gari linatumia radio waves kuzalisha nishati bila kuhitaji plugs au charging stations.
Gari linaweza kuzalisha umeme wa nyumbani – Linatoa hadi 15kW ya umeme wa nyumbani wakati likiwa limeegeshwa.
Muda usio na kikomo wa safari – Hakuna haja ya kubadilisha au kuchaji betri, hivyo kupunguza gharama za uendeshaji.
Uwezekano wa kuleta mapinduzi katika sekta ya Electric Vehicles (EVs) – Teknolojia hii inaweza kuondoa utegemezi wa lithium-ion batteries zinazotumika kwenye magari ya umeme ya sasa.
Mikakati ya utengenezaji wa ndani – Chikumbutso anashirikiana na kampuni ya China kujenga kiwanda cha utengenezaji wa magari haya nchini Zimbabwe.

Je, Teknolojia Hii Inafanya Kazi Vipi?

Chikumbutso anadai kuwa gari lake linatumia radio frequency energy kuendesha motor ya umeme (electric motor) kwa muda usio na kikomo. Hii ina maana kwamba betri ya gari huendelea kujichaji yenyewe bila hitaji la vyanzo vya nje vya nishati.

Vipengele Muhimu vya Gari

🔹 160 kW electric motor – Inaweza kutoa 320–380 Nm of torque, sawa na magari mengi ya kisasa ya umeme.
🔹 15 kW power output – Gari linaweza kutumika kama chanzo cha umeme kwa nyumba au biashara ndogo.
🔹 Self-recharging system – Hakuna haja ya kutumia charging stations au kubadilisha betri.

Changamoto na Mjadala wa Kisayansi

Ingawa teknolojia hii inaonekana kuwa mapinduzi makubwa, wanasayansi wengi wameeleza wasiwasi wao. Kulingana na Laws of Thermodynamics, haiwezekani kuzalisha nishati kutoka "hewa" bila kupoteza sehemu ya nishati hiyo katika mchakato wa matumizi.

Chikumbutso anadai kuwa alipowasilisha uvumbuzi huu kwa mamlaka za patent nchini Marekani, waliukataa kwa sababu unakiuka "kanuni za msingi za fizikia."

Hii imefanya uvumbuzi wake kuwa wa utata, huku wengine wakimtaka athibitishe teknolojia hii kupitia majaribio huru ya kisayansi.

Athari Kwa Sekta ya EVs na Nishati Duniani

Ikiwa teknolojia hii itaweza kuthibitishwa na kusambazwa kwa wingi, inaweza kuleta athari kubwa katika sekta ya magari na nishati kwa ujumla:

🚗 Mapinduzi katika sekta ya EVs – Hakutakuwa na haja ya lithium-ion batteries na charging stations.
🔋 Kupunguza utegemezi kwa madini ya nadra – Sekta ya betri inategemea lithium, cobalt, na nickel, ambayo uchimbaji wake una athari kubwa kwa mazingira.
🌍 Kuimarisha nafasi ya Zimbabwe kwenye ramani ya teknolojia ya dunia – Uwekezaji mkubwa unaweza kuelekezwa Zimbabwe kama teknolojia hii itathibitishwa.

Mustakabali wa Uvumbuzi Huu

Kwa sasa, changamoto kubwa inayokumba Chikumbutso ni:
  • Uthibitisho wa kisayansi – Teknolojia hii inapaswa kufanyiwa majaribio huru ili kuthibitisha uhalali wake.
  • Kutengeneza na kusambaza kwa wingi – Uwezo wa Zimbabwe kuzalisha magari haya kwa kiwango kikubwa bado ni changamoto.
  • Kushinda vikwazo vya kisheria na hati miliki – Teknolojia hii inaweza kukumbwa na changamoto za intellectual property rights kimataifa.
  • Kupata uwekezaji wa kimataifa – Wafadhili na wawekezaji wanahitaji uthibitisho wa kisayansi kabla ya kuwekeza kwenye mradi huu.

Hitimisho: Je, Hii Ni Mapinduzi au Udanganyifu?

Gari la umeme linalojiendesha bila kuchaji ni wazo la kimapinduzi linaloweza kubadili sekta ya magari na nishati milele. Ikiwa teknolojia hii ni halali, inaweza:

Kupunguza utegemezi wa mafuta na betri za gharama kubwa
Kuongeza usambazaji wa nishati mbadala
Kufanya usafiri wa umeme kuwa nafuu na endelevu kwa kila mtu

Hata hivyo, wasiwasi wa kisayansi unazidi kuongezeka, na inasalia kuwa suala la muda kabla ya uvumbuzi huu kuthibitishwa au kupingwa kwa ushahidi wa kisayansi.

Kwa sasa, macho ya dunia yako Zimbabwe, wakisubiri kujua iwapo Maxwell Chikumbutso atakuwa mvumbuzi aliyebadilisha ulimwengu wa magari ya umeme au la.


View: https://youtube.com/shorts/-SYzs3VMDko?si=41mDJDNt2kThqMfz


View: https://youtu.be/tClLh4VRH7A?si=djG60XwyYHsLCvJH


View: https://youtu.be/njzh1UNdwQA?si=4wSdRPSYM79q2-p9


View: https://youtu.be/yylc6VUDUZw?si=lqPlmj9O9_xAK0L6



View: https://youtu.be/lNFNqoyDheo?si=ShlSe4ViHiUQixs7


View: https://youtu.be/qEfWOSgCjnw?si=xm-DSwZcoPVQiyQU


View: https://youtu.be/GZj1smKAQy0?si=Lx0jQPN5v4GBgYEC




View: https://youtu.be/oG0tBJ4bxSs?si=Y6o2uAOa3RV6HoPe



View: https://youtu.be/B4ciYCo3cVQ?si=eIXTCAHryX3pGglZ

Max akamate hati miliki ya huo uvumbuzi kabla akina tesla and co , wasije zalisha gari kama hilo wakadai lakwao
 
Kwahio kwanini wasitupe sisi huku au lisitumike Afrika ?!!! Yaani USA ndio wanatoa Leseni za Madereva huku kuendesha ?!!

Kwa hizi logic no wonder mpaka leo watu wanashikana uchawi... cura te ipsum (Physician, heal thyself..., Yaani Mtu unakufa na kiu alafu uniambie una dawa ya kubadilisha hewa kuwa maji.., Nikikuamini lazima nikapimwe akili.
 
Hakuna kitu hapa. Ni wajinga wachache wana-share propaganda za kujiliwaza tu ili ionekane kama mwafrika anaonewa. Kwanza habari yenye haingii akilini kwa mtu mwenye kuijua dunia. Hivi ukigundua kitu kama hicho utaomba ''vibali'' kutoka kwa wazungu? Si unatengeneza magari yako na kuyauza hata nchini kwako?
Kama ni kweli angeweza kuuza hata idea yake kwao,hiyo yatosha kumpatia hela nyingi tu,,kuna wengi ufanya hivyo.
 
atengeneze, aendeshe yeye mwenyewe kama kwa mwaka hivi. watu wanaogopa sio unauzia watu afu linalipuka kama bomb, gari yenyewe ya umeme.
 
Back
Top Bottom