Afrobarometer: Idadi ya wanaotaka utawala wa kijeshi ni kubwa kuliko wanaotaka demokrasia

Afrobarometer: Idadi ya wanaotaka utawala wa kijeshi ni kubwa kuliko wanaotaka demokrasia

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Tafiti za Afrobarometer zimeonesha chini ya 50% ya Waafrika Kusini wanapendelea demokrasia kuliko aina nyingine za utawala. Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 25 ya tafiti nchini Afrika Kusini, idadi ya raia wanaounga mkono utawala wa kijeshi ni kubwa kuliko wale wanaoupinga. Karibu nusu ya washiriki wangesema wanakubali jeshi kuchukua mamlaka ya kuongoza nchi.
1761073363914.webp

Takriban watu saba kati ya kumi nchini Afrika Kusini hawaridhishwi na jinsi demokrasia inavyofanya kazi nchini humo. Waafrika Kusini maskini, wasiokuwa na ajira, na wale wa makamo wanaonyesha viwango vya juu zaidi vya kutoridhika.

Ukosefu wa ajira umetajwa kama tatizo kuu linalohitaji hatua za serikali, kwa mujibu wa zaidi ya nusu ya Waafrika Kusini. Kipaumbele kinachofuata kwa raia ni uhalifu na usalama, upatikanaji wa maji, miundombinu/barabara, na rushwa.

Watu wanne kati ya kumi wanaamini kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) imekuwa na ufanisi katika kutatua matatizo makubwa ya nchi, ingawa idadi sawia haikubaliani na hoja hiyo.
 
Back
Top Bottom