Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Mkuu Geza hili la korosho Mh. Raisi naona kama alifanya maamuzi ya jaziba na hasira. Kama alimpa muda Mh. Waziri mkuu na kabla ya muda kwisha akazuia kabaisa hao walio ahidi kununua korosho kwa bei nzuri wasiuziwe pia.
Matokeo yake serikali ikanunua kwa bei ya chini kidogo ya hizo kampuni ulizozitaja hapo juu. Pia kuhusu ubanguaji imekuwa mzigo mkubwa kwa serikali.
Mimi namuelewa sana Mh. Magufuli na ni mtetezi wake mkubwa lakini wenye ukweli lazima nisimame upande wa ukweli, mzee hapa kakosea tena sana. Nahisi atavuruga sana mtiririko wa kilimo cha korosho na soko lake.
Pia ameshajenga taswira kwamba bidhaa zetu sio za kutegemewa sana kwani mfanyabiashara akikopa pesa benki kwa ajili ya kuja kununua korosho au mazao mengine Tanzania anaweza kukumbana na maamuzi ya ghafla kama haya ya korosho mwaka huu akajikuta anafilisika kwa madeni ya fedha alizokopa bank.