Afungwa Kifungo cha Maisha Baada ya Kulipiwa Umeme (Luku) kwa Simu ya Magaidi

Nafikiri kuna ushahidi Mwingine zaidi ha huu ulioeleza hapa.

Haitoshi kumtia mtu hatiani.

Simu ya Njoroge, Mita ya Umeme ya Njoroge na Namba ya Nyumba ya Njoroge.

Yaani simu itumike kwenye uharifu badala ya kuiharibu yeye anaiuza tena?

Huyo Gaidi gani hajielewi
 
Wangekuwa wachunguzi wa nchi ya Namibia hata wasingejisumbua kufika kote huko. Angekamatwa mtu mmoja ambaye hahusiki kabisa, kisha kupewa kesi zote kuanzia kupanga hadi kutekeleza, halafu anaunganishwa na watu wake wa karibu wanaokunywaga bia pamoja.

Wale watu akili zipo kwenye mafuta ya tumboni.
 
Napenda kufanya mambo yanayonihusu kwa simu yangu, hata kutuma pesa sipendi kumwambia wakala amuwekee mpokeaji moja kwa moja, ni kheri nikatwe kiasi kadhaa ila pesa niitume kwa namba yangu mwenyewe.
Upo sahihi sana. Ila kuna mazingira inakulazimu usitumie namba yako
° Mimi situmii namba yangu mfano ninavyotuma nauli natumia kwa wakala .
° Watu wa jamii hiyohiyo ya kupewa nauli huwa nawasiliana kwa namba ambayo hata wakiangalia kwenye usajili haioneshi majina ili kuepuka usumbufu kikiwaka upande wa pili wasinijue jina.
 
Hadithi njoo uongo njoo utamu kolea
 
Naamini huyo mwenye nyumba alikuwa ni mmojawapo katika kufanikisha huo ugaidi.
 
Vipi kama mnunuaji wa hizo token alikosea,akanunua token za huyo muhusika?

Watamuamini?
Huo uchunguzi hauwezi kuwa uliishia kugundua tu kuwa alinunuliwa luku. Hiyo lazima ilikuwa ndio lead clue ya kuvumbua connection iliyokuwepo kati yake na magaidi.

Sababu kuu inaweza kuwa ni kununuliwa LUKU lakini ndio iliyopelekea kuhusishwa na tukio kwakupelekea kupatikana kwa ushahidi mwingine zaidi.
 
Inawezekana mkuu, labda kwa vile mimi nilijielekeza zaidi kwenye hiyo connection ya kununuliwa umeme, kwa ajili ya kutoa tahadhari kwa wana JF wenzangu.

Ova
 
Nilikuelewa mkuu, na comment yako imeongeza tafakari ya mjadala huu. Nimekusoma vizuri.

Ova
Yes mkuu. Kwamaana ninyingine hiyo simu yawezekana ilifanya mawasiliano mengi na miamala mingi tu lakìni mwisho wa siku huo wa LUKU ulifungua njia kupatikana mhusika mwingine kwa ushahidi wa huko mbele zaidi.

Yawezekana kuna waliotumiwa hela na hiyo simu lakini hiyo miamala haikuwa linked na tukio so huwezi kusikia wakihusishwa japo lazima walichunguzwa na kuwa cleared.

Najaribu tu kuelewesha wasiokuwa na uelewa juu ya kazi za detectives.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…