Afungwa Kifungo cha Maisha Baada ya Kulipiwa Umeme (Luku) kwa Simu ya Magaidi

Story nzuri, uandishi mzuri.

Lakini natamani kufahamu zaidi, utetezi wake ulikuwaje? Aliongelea vipi suala hilo?

Japo nimewahi kuambiwa na mtaalam mmoja wa hizi kazi kuwa kila mhalifu huacha alama, na hii ndio ilikuwa alama yenyewe.
Mimi niki host mtu apartment zangu bila kujua kama gaidi...akalipa umeme kama mpangaji tu mimi nakuwa mtegoni kwa nini ? Naona mimi ni shahidi tu hapo
 
Ninaamini kuna maelezo mengi zaidi yaliyomfanya afungwe na sio ulichoeleza peke yake.
Yes yapo mengi, jamaa alikuwa mshiriki ukiisoma hukumu utaona hilo. Mleta mada kaamua kurahisisha sana ili tu kuteka hisia za wasomaji kuwa kosa dogo kama hilo laweza kukutia matatani. Ila ukweli ni kuwa jamaa huyo mtiririko wa mambo ulikuwa mkubwa uliomuunganisha katika kesi na kuonesha alikuwa anafadhili na kuishiriki mipango ya njama hiyo ya mauwaji ya kujitoa mhanga.

Kuna wengine ambao ushahidi mdogomdogo kama huo uliwagusa ila badala ya kuwa washtakiwa walikuwa mashahidi wa upande wa mashitaka. Hii inaonesha ni jinsi gani kama hukuwa sehemu ya njama hawakuwa na sababu ya kukuingiza tu katika kesi ili kukuangushia jumba bovu.
 
Vipi kama mnunuaji wa hizo token alikosea,akanunua token za huyo muhusika?

Watamuamini?
mambo sio marahisi namna hiyo,umeme ukiishanunuliwa huwa unatumika.usipotumika system itautambua kama ni kiporo hata miaka kadhaa mbele.

sasa kama ulikosewa na bado ukaingizwa kwenye metre box yako,inabidi utolee maelezo ilikuwaje.

ndio maana ni lazima namba inayonunua umeme ndiyo ipokee token,sasa ndugu yetu alitumiwa akaweka mwenyewe au magaidi walikuwa na ukaribu na metre box yake.
 
Shambulio la mwaka 1998 Yuesi Embassy, wazee wakaingia mtaani kutafuta wahalifu wanaohusika, wakakamata watu sehemu tofauti jijini wanaosadikika kuhusika.

CIA walipofika kujiridhisha ile kuwatizama tu wale raia waliokamatwa, jamaa wakasema hatuoni gaidi hata mmoja hapa😂.
Ni wale walevi, wezi na wanywa gongo.😂.
Bongo sio poa.
Hizi story huwa mnapeana wapi? Nimecheka sana
 
Mimi niki host mtu apartment zangu bila kujua kama gaidi...akalipa umeme kama mpangaji tu mimi nakuwa mtegoni kwa nini ? Naona mimi ni shahidi tu hapo
Kesi kubwa kama hiyo ya ugaidi haiwezi kuwa rahisi mtu kuhusishwa kiholela, lazima mamlaka zimejiridhisha pasi na shaka ushiriki wake mpaka apewe hukumu hiyo.
 
Nilikuwa najikumbusha thread inayohusu hilo tukio.
Eti polisi wa bongo waliwakamata watu kibao wakawasweka central. FBI walivyofika wakaambiwa kuna watuhumiwa wa ugaidi wapo ndani, jamaa wakasema tunaomba tuwaone.
Jamaa kuwaona wakasema hakuna gaidi hata mmoja hapa labda vibaka.

Jamaa walivyoingia kazini sasa ndio wakawanasa wahusika wote na jinsi mpango mzima ulivyosukwa na kuna jamaa wa kimara huyo alishirikishwa bila kujua.
🤣🤣Bongo hakuna Detectives njaa tu na ugali ,mwenye huo uzi mkuu apasie tuupitie
 
Hizi story huwa mnapeana wapi? Nimecheka sana
Hio mbona ipo wazi, namnukuu huyu askari.

“Baada ya Ubalozi kulipuliwa sisi polisi tulifanya kazi moja tu. Hatukufanya uchunguzi, ila hatua ya kwanza ilikuwa ni kukamata kila aliyekuwa jirani na Ubalozi, aliyepita au tuliyemwona anapepesa macho. Baada ya siku tatu mahabusu za Central Polisi, Oysterbay na Salender zote zilijaa watuhumiwa. Ilikuwa hawana hata mahala pa kukanyaga, maana tulikuwa tunakamata kila tuliyemshuku.

“Baadaye walikuja askari wa FBI kutoka Marekani. Wakasema mbona mmekamata watu wengi hivi? Tukawaambia tunawashuku. Wakasema hapana. Haki za binadamu haziendi hivyo. Hapaswi kukamatwa mtu kwa kumshuku, bali mtu anakamatwa baada ya kufanya uchunguzi na kupata ushahidi usiotiliwa shaka. Tukawauliza sasa tufanyeje?

“Wale FBI walisema leteni meza hapa nje. Tukapeleka meza. Wakasema waiteni wote wanaotuhumiwa mliowakamata kisha apite mmoja mmoja tutawaambia nani ni gaidi au ameshiriki kulipua ubalozi. Tukaweka meza, tukawaita watuhumiwa wakapita mmoja baada ya mwingine. Walikuwa wengi kweli. FBI baada ya zoezi lile wakasema waachieni wote hawa hakuna mtuhumiwa hata mmoja. Tukawauliza, tukiwaachia tutaanzia wapi upelelezi? Wakatwambia waachieni tu, tutazungumza. Tukawaachia.

“Tulipoingia kwenye kikao, wakasema wale wote mliowakamata hawajui lolote katika tukio la kulipua Ubalozi. Wakatuuliza tunaweza kupata askari anayelifahamu vizuri Jiji la Dar es Salaam? Tukawaambia ndiyo. Wakasema mleteni. Akaletwa (jina linahifadhiwa) kutoka makao makuu. Wakamuuliza unafahamu eneo linaloitwa Kimara? Akasema ndiyo. Wakasema tupeleke.....
 
Story nzuri, uandishi mzuri.

Lakini natamani kufahamu zaidi, utetezi wake ulikuwaje? Aliongelea vipi suala hilo?

Japo nimewahi kuambiwa na mtaalam mmoja wa hizi kazi kuwa kila mhalifu huacha alama, na hii ndio ilikuwa alama yenyewe.
No kuna wahalifu ambao ni super world class hawaachi alama. Kuna matukio mengi tu hapa duniani mpaka leo hayachunguziki wapelelezi wa kimataifa wamekosa link (alama)
 
Nilikuwa najikumbusha thread inayohusu hilo tukio.
Eti polisi wa bongo waliwakamata watu kibao wakawasweka central. FBI walivyofika wakaambiwa kuna watuhumiwa wa ugaidi wapo ndani, jamaa wakasema tunaomba tuwaone.
Jamaa kuwaona wakasema hakuna gaidi hata mmoja hapa labda vibaka.

Jamaa walivyoingia kazini sasa ndio wakawanasa wahusika wote na jinsi mpango mzima ulivyosukwa na kuna jamaa wa kimara huyo alishirikishwa bila kujua.
Mwanasiasa anafunguliwa kesi ya ugaidi pasipo hata kufikiria inaleta picha gani kwa dunia, wakati huo huo wapo kutangaza utalii, hao watalii watakwenda mahala kuna magaidi?

Bongo balaa..
 
Wangekuwa wachunguzi wa nchi ya Namibia hata wasingejisumbua kufika kote huko. Angekamatwa mtu mmoja ambaye hahusiki kabisa, kisha kupewa kesi zote kuanzia kupanga hadi kutekeleza, halafu anaunganishwa na watu wake wa karibu wanaokunywaga bia pamoja.

Wale watu akili zipo kwenye mafuta ya tumboni.
Tangulia Central ukiwa umeweka mikono juu mwendo wa mateka kabla hawajaanza kumsumbua Melo.

🤣🤣🤣🤣
 
Hio mbona ipo wazi, namnukuu huyu askari.

“Baada ya Ubalozi kulipuliwa sisi polisi tulifanya kazi moja tu. Hatukufanya uchunguzi, ila hatua ya kwanza ilikuwa ni kukamata kila aliyekuwa jirani na Ubalozi, aliyepita au tuliyemwona anapepesa macho. Baada ya siku tatu mahabusu za Central Polisi, Oysterbay na Salender zote zilijaa watuhumiwa. Ilikuwa hawana hata mahala pa kukanyaga, maana tulikuwa tunakamata kila tuliyemshuku.

“Baadaye walikuja askari wa FBI kutoka Marekani. Wakasema mbona mmekamata watu wengi hivi? Tukawaambia tunawashuku. Wakasema hapana. Haki za binadamu haziendi hivyo. Hapaswi kukamatwa mtu kwa kumshuku, bali mtu anakamatwa baada ya kufanya uchunguzi na kupata ushahidi usiotiliwa shaka. Tukawauliza sasa tufanyeje?

“Wale FBI walisema leteni meza hapa nje. Tukapeleka meza. Wakasema waiteni wote wanaotuhumiwa mliowakamata kisha apite mmoja mmoja tutawaambia nani ni gaidi au ameshiriki kulipua ubalozi. Tukaweka meza, tukawaita watuhumiwa wakapita mmoja baada ya mwingine. Walikuwa wengi kweli. FBI baada ya zoezi lile wakasema waachieni wote hawa hakuna mtuhumiwa hata mmoja. Tukawauliza, tukiwaachia tutaanzia wapi upelelezi? Wakatwambia waachieni tu, tutazungumza. Tukawaachia.

“Tulipoingia kwenye kikao, wakasema wale wote mliowakamata hawajui lolote katika tukio la kulipua Ubalozi. Wakatuuliza tunaweza kupata askari anayelifahamu vizuri Jiji la Dar es Salaam? Tukawaambia ndiyo. Wakasema mleteni. Akaletwa (jina linahifadhiwa) kutoka makao makuu. Wakamuuliza unafahamu eneo linaloitwa Kimara? Akasema ndiyo. Wakasema tupeleke.....
Umeitoa wapi nikaisome yote? Maana huko inakoendelea ndiko pazuri zaidi.
 
No kuna wahalifu ambao ni super world class hawaachi alama. Kuna matukio mengi tu hapa duniani mpaka leo hayachunguziki wapelelezi wa kimataifa wamekosa link (alama)
Wapelelezi kukosa alama haina maana hakuna alama. Huenda wamepuuzia alama ndogo, au hawakuweza kuzingudua hizo halama.
Lakini, kila tukio huacha alama.
 
Back
Top Bottom