Afungwa Kifungo cha Maisha Baada ya Kulipiwa Umeme (Luku) kwa Simu ya Magaidi

Afungwa Kifungo cha Maisha Baada ya Kulipiwa Umeme (Luku) kwa Simu ya Magaidi

Funzo la hii story ni kuwa makini na simu yako
Halijabase sana juu ya njoroge anahusika au hausiki
Lengo ni kutaka kuonyesha tu nijinsi gani jambo dogo kama kununua Luku kunaweza kukuponza na kupelekea kupatikana ushahidi

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Story nzuri, uandishi mzuri.

Lakini natamani kufahamu zaidi, utetezi wake ulikuwaje? Aliongelea vipi suala hilo?

Japo nimewahi kuambiwa na mtaalam mmoja wa hizi kazi kuwa kila mhalifu huacha alama, na hii ndio ilikuwa alama yenyewe.
Despite your good looks, sweetness and charm you are intelligent.

Secret admirer!
 
Kuna watu wamesomea hizo kazi na wanajua namna ya kutoacha alama. Nazungumzia kama Proffessional Killers nk
Nadhani hujanielewa, nasisitiza hakuna uhalifu usioacha alama. Kila tukio la kihalifu lina alama, ni kazi na weledi wa wapelelezi vinavyohitajika kugundua alama hiyo/hizo.
 
Funzo la hii story ni kuwa makini na simu yako
Halijabase sana juu ya njoroge anahusika au hausiki
Lengo ni kutaka kuonyesha tu nijinsi gani jambo dogo kama kununua Luku kunaweza kukuponza na kupelekea kupatikana ushahidi

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Ni mbinu inatumika muda sana kutafuta simu zilizoibiwa, uhalifu n.k hasa kama ulishatumia kununua token za umeme.

Ukinunua token za umeme IMEI na namba ya simu na mita namba ya mita inabaki kwenye database zao.

Shirika la umeme linafahamu kila mita ya umeme ipo eneo lipi kwa sababu wamezifunga wao.

Ku trace kwa kutumia minara ni ngumu, simu inaweza kamata network na ipo kwenye 2G inafika hadi maximum 35km.

Wanaweza tambua location ya simu tokana na mnara wanaotumia lakini exactly location ni ngumu, inayoweza kutoa exactly location ni GPS pekee labda na ile njia ya triangulation lakini nayo ni effective ku trace magari, ndege na boats hasa katika maeneo ya wazi, lakini ku triangulate mtu katika makazi ambapo kuna msongamano wa vitu its much more difficult process.
 
Unakumbuka tukio la kigaidi lililotokea Kampala, Uganda wakati wa mechi ya fainali ya World Cup 2010, kati ya Spain na Holland?

Tukio lile lilimfanya mtangazaji wa Radio Salaam FM ya Mombasa, Habib Suleiman Njoroge kuingizwa kwenye kesi ya ugaidi wa tukio lile, na sasa anatumikia kifungo cha maisha.

- Unajua Ilikuwaje?

Mara tu baada ya lile tukio, vikosi vya upelelezi vya MI6 na FBI ni miongoni mwa vikosi vilivyoalikwa ili kufanya uchunguzi, kwa ajili ya kufanikisha kuwanasa wahusika wote.

Jambo la kwanza waligundua mabomu yote yaliyotumika katika tukio lile yaliundwa Mombasa nchini Kenya, na yakasafirishwa kwa basi hadi Malaba, mpakani mwa Kenya na Uganda.

Kisha, Mtanzania (Seleman Hijar Nyamandondo) aliyasafirisha hadi Kampala kwa gari aina ya Land Qruiser (Pickup) na kuyafikisha kwa aliyekuwa Msuka Mipango Mkuu, Issa Ahmed Luyima.

- Alivyoingizwa Mtangazaji!

Vikosi hivyo vya uchunguzi vilibaini, moja ya simu (device) zilizowasiliana na waliolipua mabomu yale, bado ilikuwa ikitumika huko maeneo ya Ukambani, nchini Kenya kwa namba tofauti na ya awali.

Kazi ya kuisaka simu hiyo ikaanza na ikanaswa ikiwa mikononi mwa mchuuzi wa sokoni, Mohamed Adan Abdow naye akiuziwa na Mtanzania, Husein Agade huku akiwa sokoni hapo.

Baada ya simu (device) hiyo kunaswa na kufanyiwa uchunguzi ikagundulika kwamba, iliwahi kufanya huduma ya kununua umeme (kama Luku), wa mita ya nyumba anayoishi mtangazaji huyo, Njoroge iliyopo Mombasa.

Hilo liliwatosha wachunguzi hao kuamini kwamba magaidi hao waliishi kwenye nyumba ya Njoroge wakati wakiunda mabomu hayo na ndiyo maana waliwajibika kulipa bili ya umeme.

- Funzo Kuu
Hiki kilichotokea kwa mtangazaji, Njoroge ni kama ambavyo mhalifu yeyote angelipia kisimbuzi chako au umeme wa mita yako kwa simu yake na moja kwa moja ukaingizwa mtegoni, endapo simu yake itachunguzwa.

Hivyo, si vema kupokea huduma za kulipiwa vifaa vyako vya nyumbani pasipo kumjua vizuri unayemwomba akulipie.

Ova
Hapo umefupisha sana, wenzetu huwa hawaconclude tu na kuishia hapo, bali wanaenda mbele zaidi, maana katika malipo unaweza kukosea namba na kumlipia mwingine

Ila huwa wanachunguza zaidi, je hiko kifaa kilikuwa eneo hilo au karibu na hilo kwa muda gani, ishawahi kuwasiliana na namba za watuhumiwa wengine n.k n.k
 
Back
Top Bottom