SoC01 Afya ya akili: Jinsi ya kutambua na kujikinga na magonjwa ya akili

SoC01 Afya ya akili: Jinsi ya kutambua na kujikinga na magonjwa ya akili

Stories of Change - 2021 Competition

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Posts
20,178
Reaction score
39,641
Katika mada iliyopita tulijaribu kuangalia ni jinsi gani jamii ina mchango mkubwa katika kuwasaidia watu wenye matatizo ya ugonjwa wa akili , pia tulijaribu kuonyesha ni kwa namna gani magonjwa ya akili hutokea na mwisho tuliona kwamba magonjwa ya akili sio ukichaa uliopitiliza tu bali magonjwa mengine kma vile sonona na mengine mengi

Kwa kiasi kikubwa tuliona ni namna gani jamii ipo karibu sana na kuwasaidia watu hawa wenye magonjwa ya akili kwamba Jamii inapaswa kuwaonyesha upendo, isiwatenge wala isiwanyanyapae. Hali kadhalika jamii iwe na utaratibu wa kuwasaidia katika mahitaji yao ya msingi ikiwa ni pamoja na kuwapeleka kupata huduma

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya mwaka 2019, kila sekunde 40, mtu mmoja hupoteza maisha kwa kujiua. Hii ina maana kwamba kila mwaka watu takribani 800,000 hufa duniani kote kwa kujiua. Hili ni tatizo ambalo linaonekana kuongezeka mwaka hadi mwaka. Ukweli ni kwamba, tatizo hili halizungumzwi vya kutosha miongoni mwa jamiina hasa katika jamii yetu ya kitazania , na katika mada ya leo tutaonana sasa namna ya kutambua magonjwa haya na( binafsi au kwa mtu mwingine na namna ya kujikinga nayo )

Tunaposema mtu mwenye akili timamu huwa tunamaanisha nini haswa ?
Mtu mwenye akili timamu ni mtu mwenye kukamilika kiakili. Mtu huyu anakuwa na uwezo wa kujitambua, kufikiri, kuelewa, kukumbuka, kuwasiliana na kushirikiana na wengine, kujifunza, kupanga, kujisimamia katika shughuli zake za kimaisha, kuhimili na kutatua changamoto za kimaisha kwa kutumia akili na maarifa.

Dalili kubwa zinazoweza kutuonyesha matatizo katika mfumo wa fahamu kwa ujumla ni kama zifuatavyo , ni vizuri kufahamu pia kwamba dalili hizi zitathibitika iwapo tu zitajitokeza mfululizo na kudumu kwa zaidi ya wiki mbili

1. KUJIHISI MCHOVU MARA KWA MARA , hii hali huendana na mabadiliko ya kihisia kujihisi mnyonge kwa muda mwingi.

2. KUPOTEZA HAMU YA VITU ULIKUA UNAVIPENDA MWANZO , mfano mwanaume ulikua unapenda mpira unakua unaona hauna haja tena .

3. MABADILIKO KATIKA USINGIZI , usiku unakua unashindwa kulala na mchana ndo unakua muda wako wa kusinzia hivyo kuathiri shughuli zako mbali mbali za kijamii .

4. MABADILIKO KATIKA ULAJI WA CHAKULA , kula sana au kula kidogo sana .

5. KUJIONA HUNA THAMANI , NA KUJITENGA NA WENZAKO MARA KWA MARA

6. MWISHO NI KUWA NA HASIRA ZA MARA KWA MARA NA BILA SABABU YA MSINGI

Hizi ni miongoni mwa dalili kuu ambazozinaweza kutuonyesha kwamba mtu huyu ana tatizo katika mfumo wake wa akili na huonyesha dalili hizi kwa muda wa zaidi ya wiki mbili au zaidi katika jinsi ya kupambana namagonjwa ya akili leo tutaangalia zaidi jinsi ya kupambana na msongo wa mawazo maana hili ndo tatizo kubwa tulilo nalo watanzania
zifuatazo ni baadhi ya njia chache zinazoweza kukusaidia kupambana na msongo wa mawazo msongo wa mawazo huwa upo kuna muda tunakumbwa na mambo tusiyoweza kuyatawala ila ni muhimu sana kuhakikisha mambo hayo hayaathiri afya yetu ya akili tunaweza fanya hivyo kwa

1. EPUKA MAWAZO HASI KUHUSU WATU AU JAMII , ni vyema kila mtu kujifunza kuyachukulia mambo katika mlengo chanya hata jambo baya likitokea tambua litapita na kuna namna ya kulitatua ukituliza akili

2. PATA LISHE BORA NA JIHUSISHE NA MAZOEZI MACHACHE , katika mada iliyopita tuliona kwamba kwenye mwili kuna kemikali ambazo zinajihusisha na kusafirisha taarifa kwenye ubongo hivyo zinapopungua mtu anaweza pata haya magonjwa ya akili mazoezi ni kiungo muhimu sana kwani huimarisha usafirishaji wa hizi kemikali mwilini vyakula vya nyuzi nyuzi kama vile matunda na mboga za majanini muhimu sana kwa afya akili pia samai zenye omega 3 tofauti na vyakula vya mafuta

3. PUUZIA MAMBO YANAYOWEZA KUKUUMIZA NA JIWEKE NAYO MBALI , kama umekosa utatuzi katika jambo flani au na mtu flani vizuri kujitenga na hicho kitu kukiweka mbali , mada iliyopita tuliona jinsi maneno mabaya yanaweza sababisha ajali katika mifumo ya usafirishaji wa kemikali katika bongo zetu , majasusi huwa wana msemo wa '' get out of x '' jiepushe na jiweke mbali

4. KUTAFUTA SHUGHULI MBADALA NA ILE UIFANYAYO KILA SIKU , kufanya shughuli mpya husaidia kwa kuuletea ubongo changamoto mpya ambayo ubongo utabidi uwe makini katika kujifunza ( concentration ) hivyo kuyachepusha mawazo , sio kwamba mawazo yatapotea kabisa ila unavyofanya mara kwa mara ndivyo ubongo unazoea

5.Eleza tatizo ulilonalo linalokusababishia msongo wa mawazo kwa mtu aliye karibu nawe yaani mtu unayemwamini kuwa atakuwa tayari kukusikiliza.Hatua hii husaidia kuondoa hisia hasi kutoka moyoni ,usizihifadhi hisia hasi kwani zitazidi kuongezeka na mwisho zitaharibu afya yako ya akili. Kaa karibu na watu uwapendao

MWISHO kabisa pata msaada wa kitaalamu toka kwa sisi wataalamu wa afya ila kama kuna msaada zaidi uweze kusaidiwa

Nimalizie kwa kusema kwamba serikali inapaswa iongeze mwamko katika swala zima la afya ya akili ihakikishe elimu inatolewa mashuleni na katika jami nzima kwa ujumla pia wadau wa sayansi na teknolojia watengeneze applications zinazoweza kutumika kuzuia matukio mengi ya kujiua kama wenzetu wa magharibi na nchi zingine hufanya

VUNJA UKIMYA MAGONJWA YA AKILI YANATIBIKA NA KUEPUKIKA .
 
Upvote 40
YOUR SOUL NEED PEACE

Over everything try hard to have peace
 
Sometimes all you are passing through can just be worked out by having conversations with someone

Just find someone to speak with
 
Mental health…is not a destination, but a process.
 
It’s ok to take time out. Your mind too needs a break; not just your physical body. With so much going on around us, it’s easy to get caught up with things & overlook your mental health. Don’t feel guilty about having “me” time to restore your energy & refocus your mind!
 
When older people talk about depression or suicide it is important to pay attention and get them psychiatric help
Don't ignore them
 
Kwenye baadhi ya situations kama vile heart diseases
Mental health problems kama vile depression zmeonyesha kuleta matatzo zaidi na kufanya ugonjwa huo uendelee zaidi hata tukiwafanyia surgery za bypass ni ngumu sana kwa wao kupona

Depression influences blood pressure, heart rhythms, and clotting of blood in the heart
 
Stress huchangia kudorora kwa kinga ya mwili kuna stress za aina mbili stress za muda mrefu na stress za muda mfupi

Stress za muda mfupi huongeza kinga ya mwili (strength of immune response)
Na stress za muda mrefu hupunguza kinga ya mwili

Inapaswa tufahamu kuwa unapopatwa na stress kama vile unavyopata mashambulizi mengine ya mwili

Mwili hu react kwa kujilinda na kutoa kemikali mbali mbali kwa ajili ya kujilinda ( cell kama vile lymphocytes na zingine huja kufanya kazi
 
If you had a massive loss find a meaning again of you to live

The meaning of your life
 
Depressed person thoughts are focused inward rather than towards the external events
 
Wewe, mimi na jamii yote kwa jumla ni wadau muhimu katika kuchangia kupunguza matatizo ya afya ya akili. Kwa kushirikiana tunaweza kuokoa maisha ya watu wanaokaribia kujidhuru au kujiua na kuzuia uwezekano wa kuwadhuru wengine kutokana na matatizo ya afya na ugonjwa wa akili. Aidha serikali hasa watunga sera watoe kipaumbele katika kukabiliana na matatizo ya afya ya akili nchini.
 
YOUR SOUL NEED PEACE

Over everything try hard to have peace
 
Back
Top Bottom