Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Habari za leo,
Kama mnavyofahamu kuwa HIV au UKIMWI sikuhizi ni gonjwa sugu na wala si gonjwa hatari kama ilivyokuwa hapo awali (kwa wanaotumia dawa), hivyo basi ni muhimu kujua afya za watu tunawaajiri kama wasaidizi wetu nyumbani, kwakuwa sisi ni waajiri wao.
Ikitokea majibu ya dada yamekuwa negative (-ve), kwa wababa wengine ni kama vile wameambiwa hii nyama ni halali. Ikitokea majibu ni postive (+ve) kwa dunia tuliyonayo, hakuna haja ya kusitisha ajira, cha muhimu ni kumpeleka kwenye kitengo aanze matibabu. Ukiwa kama mwajiri, siri yake inabidi uihifadhi kama vile MASIJALA BAYANA na HUMAN RESOURCES wanavyohifadhi file lako. Sio dada amevunja glass unaanza, "kwanza wewe mgonjwa nime kustiri tu hapa" kama vile wewe huwezi kuvunja hiyo glass.
Kumpa support ili ahudhurie appointment zake kwenye kitengo ni kitu cha muhimu sana, siku hizo unaweza kutafuta mtu mwingine wa kukaa na watoto, pia kumsisitiza kutumia dawa zake.
Hakuna mkamilifu lakini tunaweza kuweka mapungufu yetu kuwa na jamii kamili.
Ijumaa njema,
Sky Eclat.