Afya ya wafanyakazi wa ndani

Afya ya wafanyakazi wa ndani

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Habari za leo,

Kama mnavyofahamu kuwa HIV au UKIMWI sikuhizi ni gonjwa sugu na wala si gonjwa hatari kama ilivyokuwa hapo awali (kwa wanaotumia dawa), hivyo basi ni muhimu kujua afya za watu tunawaajiri kama wasaidizi wetu nyumbani, kwakuwa sisi ni waajiri wao.

Ikitokea majibu ya dada yamekuwa negative (-ve), kwa wababa wengine ni kama vile wameambiwa hii nyama ni halali. Ikitokea majibu ni postive (+ve) kwa dunia tuliyonayo, hakuna haja ya kusitisha ajira, cha muhimu ni kumpeleka kwenye kitengo aanze matibabu. Ukiwa kama mwajiri, siri yake inabidi uihifadhi kama vile MASIJALA BAYANA na HUMAN RESOURCES wanavyohifadhi file lako. Sio dada amevunja glass unaanza, "kwanza wewe mgonjwa nime kustiri tu hapa" kama vile wewe huwezi kuvunja hiyo glass.

Kumpa support ili ahudhurie appointment zake kwenye kitengo ni kitu cha muhimu sana, siku hizo unaweza kutafuta mtu mwingine wa kukaa na watoto, pia kumsisitiza kutumia dawa zake.

Hakuna mkamilifu lakini tunaweza kuweka mapungufu yetu kuwa na jamii kamili.

Ijumaa njema,
Sky Eclat.
 
kweli ni jambo zuri, ingawa ni wachache sana watakaoweza kuwakuta +ve na kutositisha ajira yake
 
Akifika kwako mpeleke Hospital asije kuwaambukiza watoto wa kiume na Mme wako dah ndo mana House girl. Hapigwi kavu
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Habari za leo,

Kama mnavyofahamu kuwa HIV au UKIMWI sikuhizi ni gonjwa sugu na wala si gonjwa hatari kama ilivyokuwa hapo awali (kwa wanaotumia dawa), hivyo basi ni muhimu kujua afya za watu tunawaajiri kama wasaidizi wetu nyumbani, kwakuwa sisi ni waajiri wao.

Ikitokea majibu ya dada yamekuwa negative (-ve), kwa wababa wengine ni kama vile wameambiwa hii nyama ni halali. Ikitokea majibu ni postive (+ve) kwa dunia tuliyonayo, hakuna haja ya kusitisha ajira, cha muhimu ni kumpeleka kwenye kitengo aanze matibabu. Ukiwa kama mwajiri, siri yake inabidi uihifadhi kama vile MASIJALA BAYANA na HUMAN RESOURCES wanavyohifadhi file lako. Sio dada amevunja glass unaanza, "kwanza wewe mgonjwa nime kustiri tu hapa" kama vile wewe huwezi kuvunja hiyo glass.

Kumpa support ili ahudhurie appointment zake kwenye kitengo ni kitu cha muhimu sana, siku hizo unaweza kutafuta mtu mwingine wa kukaa na watoto, pia kumsisitiza kutumia dawa zake.

Hakuna mkamilifu lakini tunaweza kuweka mapungufu yetu kuwa na jamii kamili.

Ijumaa njema,
Sky Eclat.
Mada zako huwa ziko Makini sana nakupendaga hapo tu[emoji8]
 
Tatizo hawa wanaume wakijua status ya afya ya dada wanatake advantage hasa ikiwa nzuri
 
Ungeweka na mbinu za kuwapima hawa beki tatu, maana Kama unavyojua si rahisi kumshawishi mtu kucheki afya yake tena HIV, ndugu yako tu inakua tabu kumshawishi ijekuwa msichana wa kazi?
 
Wakuu katika maisha yangu nilimuomba Mungu anijalie kuwajali sana hawa wadada wakazi.Niliwahi kukaa ofisi moja na mdada alikuwa na mtoto mdogo nikawa namsikiliza anavyomgombeza mdada wa kazi machozi yalinitoka hadi nikafikia kumwambia hebu jenga picha kuwa boss anakuja hapa anakugombeza kama unavyomgomeza yeye wewe utajisikiaje akanyamaza.Hawa dada zetu ndo hao wanaandaa chakula chetu ndo hao wanajua in and out za majumbani mwetu tujaribu kukaa nao kama binadam wengine na tuchukulie ile kazi ni kama kazi nyingine.

Kazi za ndani ni ngumu hebu chukulia wewe zimekushinda ndo ukaona umtafute hivyo ni jukumu lako kumfanya na kumjali kama mwajiri wako anavyokujali.Kimsingi ukiwa na roho ya ubinadamu unaweza ukamkatia bima ya afya ili kutunza afya yake na za kwenu kwa kuwa yeye ndo anawahudumia. Mwisho Unavyotaka wewe utendewe please na wewe tenda hivyo hivyo kwa wenzako.
 
Kumuelimisha tu mkuu, hata WHO pia wanashauri kila mtu apime afya, si kwa HIV tu bali kisukari, cancer, hypertension, malaria na mengineyo. Kama akikubali yote hayo unamshauri amalizie HIV awe amepata full status.
 
Watu wanakosa utu kabisa, hawaelewi kuwa what goes around comes around, mtoto wako anaweza kuja kunyanyasika hivyo hivyo unavyonyanyasa dada wa kazi.
 
Sawa umenena vyema, lkn kwa ninavyojua hawa wataalam wetu wa afya hawawezi kutoa majibu kwa mtu mwingine tofauti na mhusika anayefanyiwa vipimo, labda mpaka mhusika alidhie wewe kuhusiswa katika majibu yake. Unafikili msichana wa kazi Kama akiwa na wasiwasi na afya yake anaweza kukubali kirahisi wewe upokee majibu ya vipimo vyake?
 
Mwelimishe kuwa hata kama majibu yatakuwa makubwa sio mwisho wa maisha, siku hizi kuna maendeleo makubwa kwenye tiba pia ni faida yake yeye wewe unajua utafanya nini hata majibu yako yakiwa mabaya.
 
huo upimaji n hiyari au lazima tuanziae hapo kwanza.?
Elimu hapa inahitajika, unajua ndiyo maana tunapata magonjwa nyemelizi kirahisi, watu wanaachia ugonjwa ushambulie mpaka kinga inashuka kabisa wakati walikuwa na chance ya kurekebisha mambo kama wangejitambua mapema.
 
Watu wanakosa utu kabisa, hawaelewi kuwa what goes around comes around, mtoto wako anaweza kuja kunyanyasika hivyo hivyo unavyonyanyasa dada wa kazi.
Hizi ni kazi kama kazi nyingine jamani tuwe na utu dunia ni mapito.
 
Back
Top Bottom