Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Afya ya wananchi ndiyo kitu muhimu kuliko vyote. Shughuli zote za uchumi wa nchi zinategemea sana afya za wazalishaji kuwa na afya njema ya kimwili, kisaikolojia, kiakili na kiroho.
Hii mifuko ya bima za afya ambazo ndiyo tegemeo kuu kwa afya za wananchi zimekuwa zikisuasua kutokana na ukata.
Haziwezi kumudu kujitegemea bila ya kuwakamua sana wateja wake, jambo ambalo haliwezekani kwani wengi wa hao wateja watarajiwa hawana cha kukamuliwa kihivyo. Huu ndiyo ukweli, tutake tusitake.
Sasa kama tunaweza kutoa ruzuku kwa maeneo mbali mbali hususani kwenye mbolea, kwa nini tusifanye hivyo kwenye mifuko hii ya bima za afya?
Tumesikia mfuko wa NHIF ukilalamika kuelemewa na gharama kubwa ya matibabu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza hususani yale ya saratani, kisukari, figo na moyo ambayo gharama zake zinafikia shilingi bilioni 99 kwa mwaka.
Kwa nini serikali kwa kuanzia isitoe ruzuku ya shillingi billion 100 kila mwaka kwa mfuko huu kutoka kwenye bajeti yake ya mwaka?
Na iendelee hivyo hivyo hadi mifuko hii itakapokuwa na uwezo wa kujitegemea kwa asilimia 100. Kupanga ni kuchagua.
Kwa heshima na taadhima naomba kuwakilisha ombi hili.