Afya yangu yazidi kunichanganya

Nimekupata mkuu
 
Nimekuelewa sana tu. Asante
 
Ventilation system unapoishi ipoje
USIJE UKAWA UNATUMIA STANDING FAN ALAFU UKAWA UNALALAMA NA KIKOHOZI
 
Pole sana,nenda ucheki vipimo vya mwili wote kwenye MRI
 
tafuta dawa inaitwa Montelukast kunywa siku 10 kila siku usiku kidonge 1! kitayeya
Umenikumbusha kitu.
👇👇👇👇👇
treating chronic asthma and prophylaxis and the prevention of exercise-induced bronchoconstriction. It is also approved to relieve seasonal and perennial allergic rhinitis
 
Pole Sana, Mimi pia napitia hali ya kikohozi nimekunywa madawa mengi ya hospitali na kienyeji lakini wapi, x-ray , makohozi, vyote vipo vizuri , asali, vitunguu nk vyote nimetumia lakini wapi
 

Habari!

Hapa kuna mifumo miwili ambayo iko karibu na inaweza kuhusika kwa pamoja kwenye dalili unazozieleza:

1: Mfumo wa chakula
2: Mfumi wa hewa
3: Maumbile karibu na mifumo husika

Kuna mambo ambayo yanaweza kuathiri mifumo yote miwili kwa wakati mmoja. Na hivyo kuweka ugumu wa kujua kipi kimeanza.

1: Mfumo wa chakula(GERD)
Hili ni tatizo ambalo linaweza kuleta athari kwenye mifumo yote miwili. Matokeo ni kushindwa kujua nani kamuanza mwenzake kwani inakuwa ni duala la dalili/ mzunguko wa dalili. Hii huweza kuanzisha kwa shida ndani ya mfumo wa chakula au nje ya mfumo husika.

2: Allergy hasa kifua
Ni tatizo ambalo linaweza kuathiri mifumo yote miwili kwa wakati mmoja. Au mmojawapo na baadaye madhira kuhamia kwingine. Kwani ukila kitu kinachoanzisha allergy, matokeo yaweza kuonekana kirahisi upande wa njia ya upumuaji lakini pia kwenye mfumo wa chakula wenyewe. Allergy ya kwenye kifua isipopata tiba sahihi huweza kuathiri uwezo wa utendaji kazi wa mapafu na dalili kuwa mara kwa mara au zisizoisha.

3: Maambukizi/shida ya kifua
Huweza kusababisha umezaji wa chakula kuwa shida, inakuwa ni suala la timing. Ukila tu kikohozi huanza. Hii pia inaweza kuhusisha maumbile nje kuzunguka mfumo wa upumuaji.

4: Dalili nyingine ni madhira/ complications
Uwepo wa shida moja kwa muda mrefu huweza pia kusababisha madhira mengine. Ambayo huongeza mchanganyiko wa dalili.

MAONI BINAFSI
Kupata mtaalamu wa afya ambaye atakupatia muda wa kutosha kujieleza na ukaguzi. Usichoke au kukata tamaa kujieleza. Pia ni muhimu kuwa na tabia ya kutengeneza faili lako la maelezo, vipimo na dawa ulizowahi kutumia na kwa muda gani.

Pia jitahidi kuandika maelezo ya jinsi tatizo lilivyoanza na dalili za mwanzo, nini kilifuata, hii utakusaidia kwenye kutoa taarifa sahihi. Mapito ya kazi, atumizi ya manukato, milo yako, historia ya familia kama allergy nk. na maisha kwa ujumla pia ni muhimu.

Baada ya kumwona mtaalamu wa kwanza
kulingana na yatakayopatikana pamoja na kuangalia/kufanya ukaguzi wa mwili kuna speciality ambazo anaweza kupendekeza uzione.

Binafsi kwa machache yaliyopo ninaona wafuatao ni muhimu wakuone pia kama uko kwenye mazingira wanayopatikana:

1: Gastroenterologist/daktari bingwa wa njia ya chakula.

2: Pulmonologist/Daktari bingwa wa mfumo wa upumuaji.

Ni muhimu kuzingatia kuwa tiba nyingi si dawa tu, bali kuzingatia mabadiliko ya mfumo wa maisha kwa kadri utakavyoelekezwa.
 
Yawezekana ukawa na gastroesophageal reflux disease Gerd
Ama allergy
Kapime madonda ya tumbo pia

Ukilala flat bila mto unapata shida
Ama kiungulia?
Au kukohoa?
 
Black Pepper Black Pepper Black Pepper Black Pepper Black Pepper
 
Nimekuelewa mkuu. Asa hao ma doctor nawapateje, make sikuhiz ma doctor niweng. Naote wamevaa sura za kidoctor
 
Yawezekana ukawa na gastroesophageal reflux disease Gerd
Ama allergy
Kapime madonda ya tumbo pia

Ukilala flat bila mto unapata shida
Ama kiungulia?
Au kukohoa?
Kiungulia xipat. Yan nikukohoa tu. Inafika sehem natumia nguvu xana kukohoa mfrulizo mpaka nahisi mbavu zinauma
 
Mkuu subir wataalamu wa mambo ya Ulozi waje.

Lazima watakuita DM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…