Aga Khan mmekosa utu na kuweka mbele maslahi kuliko huduma kwa wananchi

Aga Khan mmekosa utu na kuweka mbele maslahi kuliko huduma kwa wananchi

Political Jurist

Senior Member
Joined
Sep 6, 2021
Posts
143
Reaction score
120
Katika pita pita zangu mtandaoni nimekutana na taarifa iliyozua gumzo ambayo inahusu Hospitali ya Aga Khan kuiiomba NHIF isitishe mkataba wake wa utoaji wa huduma kwa sababu za kiuendeshaji.

Ilinistua na nikalazimika kwenda mbali zaidi ili kujua sababu ya suala hilo. Hakika niliumia sana kuona hospitali hii inalazimisha ilipwe mamilioni ya fedha na NHIF katika utoaji wa huduma zake, bei ambazo hata katika Hospitali nyinginezo tena zilizo ngazi ya juu ya rufaa ya matibabu.

Katika uchunguzi wangu nilioufanya nimebaini madudu mengi ambayo Aga Khan inataka kuibebesha Serikali mzigo wa kuongeza gharama zaidi za huduma kwa wateja wa NHIF kuliko kiwango cha juu kabisa cha malipo kwa huduma.
Nitatoa mifano michache ya huduma za kawaida kabisa ambazo Aga Khan imekuwa ikidai kuongezewa gharama hizo kwenye huduma wanazotoa kwa wateja wa NHIF.
  • Hospitali ya Aga Khan wanataka kutoza Shilingi 6,000,000/= kwa huduma za kujifungua kwa njia ya upasuaji wakati Hospitali nyingine zenye hadhi sawa ya rufaa ya Kanda wanatoza kiasi cha Shilingi 230,000/= huku bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ikijumlisha na huduma ziada hutoza kiasi cha Shilingi 600,000/=. Aga Khan wanataka kulipwa maradufu kwa asilimia 100 zaidi kuliko Hospitali nyingine.
  • Huduma ya kulaza wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Aga Khan wanataka kulipwa kiasi cha Shilingi 2,278,933, huduma hii kwenye Hospitali nyingine huwa ni kiasi cha shilingi 500,000/= na Shilingi 700,000/= ambayo ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada.
  • Aga Khan wanataka kutoza kiasi cha Shilingi 334,546 kwa huduma za uchunguzi kwa kupitia CT-Scan huku Hospitali nyingine zinatoza 120,000 hadi 150,000 ikiwa ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada. Kwanini bei iwe juu hivi? CT-Scan hizi hizi ambazo tumeona Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amezinunua na sasa huduma zinapatikana nchi nzima kwenye Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na nyinginezo ngazi za juu. Najiuliza Gharama zote hizo zinakuja kwa msingi upi?

Ifahamike kuwa Aga Khan sio Hospitali ngazi ya Taifa hivyo bado rufaa zao zote wanalazimika kuzipeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili, hata kama ni Hospitali Binafsi ukiweka gharama za juu pamoja na huduma za ziada hawapaswi kuwa na tofauti kubwa ambayo inatishia uhai wa Mfuko.
Kama Taifa ifike mahali tutafakari endapo Aga Khan wana nia kweli ya kutoa huduma za matibabu au la? Je ni wananchi wangapi wataweza kupata huduma kwa gharama hizi katika hospitali hii? Au wamelenga tabaka gani la kulitibia?

Hata hivyo niipongeze sana Serikali kwa hatua kubwa ya kuboresha huduma za matibabu nchini huduma ambazo awali yawezekana zilipatikana nje ya nchi lakini sasa zinapatikana katika hospitali zetu za umma. Kwa hili kongole kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Viongozi wa na Watendaji wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Waziri jembe kabisa Mhe. Ummy Mwalimu.

Ninaamini kwamba katika utoaji wa huduma za matibabu, utu hupaswa kuwa kipaumbele cha kwanza na kuweka maslahi mapana ya kuokoa maisha ya binadamu.

Kwa leo niwaache na tafakari hii ya gharama kubwa zisizo na uzalendo za Aga Khan.

IMG-20240814-WA0089(3).jpg
 
Sijakuelewa kwanini unawalalamikia Aga Khan nao ni private, si bora ungejaribu kulinganisha na bei za private zingine... au?

Ila nimekuelewa umeumia hautaweza kumudu dharama zao.. Kwa mifano Muhimbili pako vizuri tu.. Napo mtu unalipia kama hauna Bima pesa ndefu ikitokea mtu amekumbwa na matibabu yakumfikisha huko. Nao wana huduma na wodi za private.. Pesa yako tu..
 
Ninachojua mimi as longer as niko hai na familia yangu ”afya zetu wote ni biashara kwa wanaofanya biashara za hospital” government hospitals zikiwa included.

Mwezi wa pili mwaka huu mwanangu alipata ajali ya moto akalazwa Muhimbili pale nimeacha 2.4mill na point hakuna anayejali.
 
wana tax exemption kwa kila wanachoingiza nchini ujue.

halafu hawajawai kuwa na utu hao jamaa.
Ndiyo. Wana tax exemption.
  1. Waki import vifaa vyovyote vile, magari n.k. hawalipi ushuru
  2. Income yao hawalipi kodi
  3. Ma expatriates hawakatwi PAYE
Kama wanasitisha huduma kwa nhif, hizo tax exemption zifutwe.
 
AGA KHAN MMEKOSA UTU NA KUWEKA MBELE MASLAHI KULIKO HUDUMA KWA WANANCHI.

Katika pita pita zangu mtandaoni nimekutana na taarifa iliyozua gumzo ambayo inahusu Hospitali ya Aga Khan kuiiomba NHIF isitishe mkataba wake wa utoaji wa huduma kwa sababu za kiuendeshaji...
Mchagua jembe si mkulima.
Mgonjwa hachagui hospitalo!
Mfungwa hachagui gereza!
 
AGA KHAN MMEKOSA UTU NA KUWEKA MBELE MASLAHI KULIKO HUDUMA KWA WANANCHI.

Katika pita pita zangu mtandaoni nimekutana na taarifa iliyozua gumzo ambayo inahusu Hospitali ya Aga Khan kuiiomba NHIF isitishe mkataba wake wa utoaji wa huduma kwa sababu za kiuendeshaji...

Nenda mwananyama kajifungue Kwa elf 40

Mbona ni Jambo simple tu
 
Kwa hali ya mfumko wa bei ilivyo, nafikiri Aga Khan wako sahihi.

Haiwezekani bei za mafuta, chakula, vinywaji, nauli ya daladala n.k zipande zaidi ya mara 3 (3x) halafu dawa, huduma na vifaa vya hospitali vibakie vile vile au kupungua kama ambavyo NHIF wanapendekeza.
 
Ndiyo. Wana tax exemption.
  1. Waki import vifaa vyovyote vile, magari n.k. hawalipi ushuru
  2. Income yao hawalipi kodi
  3. Ma expatriates hawakatwi PAYE
Kama wanasitisha huduma kwa nhif, hizo tax exemption zifutwe.
Ndo nawashangaa watu hapa wanakomaza fuvu et ni private hospital, hawana ruzuku kutoka serikalini, nyenyenyenyeeee, hao jamaa hawajawai lipa kodi tangia waingie nchini, na ardhi yetu walipewa bureee, na kuna maeneo wanamiliki wala hawajayaendeleza.

WAONDOKE TU.
 
wana tax exemption kwa kila wanachoingiza nchini ujue.

halafu hawajawai kuwa na utu hao jamaa.
Aliyekosa utu ni NHIF anayetukata pesa kila mwezi na kuzitapanya bila huruma. Leo hii nikienda kwa huduma ya X-ray nalazimika kuongeza elfu 10 kasoro kidogo. Aga Khan wala ailaumiwe, mchawi mkuu ni huyu NHIF.
 
Ile ni Hospitali binafsi.Kama vipi nawe fungua yako halafu ufanyw hicho unachotaka Aga Khan wafanye.Msilete mindset za Kisisiem kwenye kila jambo
 
Aliyekosa utu ni NHIF anayetukata pesa kila mwezi na kuzitapanya bila huruma. Leo hii nikienda kwa huduma ya X-ray nalazimika kuongeza elfu 10 kasoro kidogo. Aga Khan wala ailaumiwe, mchawi mkuu ni huyu NHIF.
umeelewa mada?
 
Back
Top Bottom