Agano la Mwisho: Je, Sisi ndio waandishi wa vitabu hivyo?

Agano la Mwisho: Je, Sisi ndio waandishi wa vitabu hivyo?

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Kwa wale Wakristo watakua na ufahamu kwamba, katika kitabu kitakatifu cha Biblia kuna mkusanyiko wa vitabu vya Agano la kale na Agano Jipya.

Vitabu vya Agano la kale viliandikwa kabla ya Kuja kwa Yesu Kristo na vilitabiri na kutueleza kuhusu ujio wake.

Mtawala katika awamu hiyo Alikua Mungu Mwenyewe.

Vitabu vya Agano Jipya viliandikwa na wale waliotambulika kama wanafunzi wa Yesu.

Walieleza injili yake na namna ya kupata mafanikionya kiroho kupitia yeye.

Mtawala alikua Yesu Kristo.

Baada ya kufa na kufufuka kwa Yesu wakati Yesu anapaa kuelekea Mbinguni alitamka maneno kwamba anatuachia msaidizi wa kutushauri ambaye ni Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu ni Nafsi ya Tatu katika Uungu.

Kwa sasa Baada ya Mungu Mkuu na sasa anayetawala ni Roho Mtakatifu.

Ili uungu ukamilike na Kufikia mwisho wa Dunia hii.

Tunahitaji vitabu vitavyotokana na Roho Mtakatifu.

Sisi ndio tunaishi nyakati hizi ambazo Roho Mtakatifu anatawala.

Je, tunashuriki namna gani kuviandika vitabu vitakatifu vya Mungu?

Tambua kwamba baada ya kukusanywa kwa vitabu vitakatifu vya nyakati hizi.

Dunia itakua imefikia ukamilifu.

Itakwisha.
 
Duh, itabidi big data itumike

Iundwe programu itakayosearch madini yote kwenye makumbusho ya intaneti

Hadi humu JF wapite kukusanya
Duh, itabidi big data itumike

Iundwe programu itakayosearch madini yote kwenye makumbusho ya intaneti

Hadi humu JF wapite kukusanya
Kazi hiyo itafanywa na vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom