DOKEZO Agent wa Fedex Tanzania (Rangel Logistics) Achunguzwe kwa kuhujumu uchumi

DOKEZO Agent wa Fedex Tanzania (Rangel Logistics) Achunguzwe kwa kuhujumu uchumi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Utashangaa mfanyakazi wa kawaida tu wa FedEx Yuko njema, kumbe kuna uharamia unaendelea?
 
FedEx sio matapeli tatizo wabongo wanao wawakilisha fedEx hapa nchini
naamini FedEx Int'l wanaona reviews zilizopo kwenye ukurasa za hao agents pale Google na ni miaka sasa, hakuna hatua zinachukuliwa

kusema FedEx ni matapeli ni sahihi kabisa
 
Everything is horrible hapo nyumbani.
Kuna account inaitwa Tanzanite CRDB,nna miezi 6 Sasa wameniblock,
Fees wanalamba km kawaida,nikilalamika wanasema unblocked.
Nikijaribu kulog inn blocked again.
Ishatokea zaidi ya mara 10.
Nishakata tamaa.
Upuuzi mwingi sana.

Hii account ya Tanzanite ni utapeli mkubwa. Kinachotokea hata pesa zako zinakuwa hazipo wanachukuwa na kupeleka kuwekeza kwa miezi mitatu mitatu. Ukilalamika sana wanarudisha pesa.

Hii ni account maalumu kwa diaspora hivyo wanajua diaspora wengi wanaweka pesa na kuacha kwa muda mrefu wanavyofanya ukiweka pesa wana chukuwa pesa yako wananunulia CD za miezi mitatu mitatu na kupata faida kwa pesa zako wakati huohuo wanakulipisha kila mwezi na kupata dollar!!!.

Ushauri
1. Tafuta NIDA na fungua account ya kawaida
2. Acha pesa kidogo pesa nyingine peleka UTT na nunua bond fund ambayo itakulipa 12%-14% kwa mwaka. Hiyo account unatuma pesa halafu unaenda kwenye mtandao una move pesa kwenye account yako ya UTT na siku ukirudi nyumbani unakuwa na uwekezaji wa uhakika kwenye account yako badala ya utapeli wa CRDB

Mimi ndiyo niko kwenye utaratibu huu lakini usiseme unaishi nje sema uko nje kwa muda kwa shughuli zako lakini NIDA ni muhimu sana
 
UPS ndiyo mbaya zaidi ya FEDEX NA DHl combined. DHL wapo vizuri kwenye mifumo yao na wana respond haraka sana hata kabla mzigo haujafika wanakupa ulipie gharama zote. Shida ni DHL hawana shortcut. Kila kitu kinafuata utaratibu. Fedex kama unfahamiana na watu wawili au watatu utakuwa okay. Lakini UPS ni takataka kabisa usiombee mzigo uje na UPS. Bora kuliko wote ni SPEEDAF wa ALIEXPRESS. Hawa wanakuletea mzigo bure kabisa hadi mlangoni na huchajiwi sentano ya kodi, au chochote. Posta sasa hivi biashara ya vifurushi imedoda kabisa sababu SPEEDAF kateka soko lote la vifurushi kutoka China kupitia ALIEXPRESS.
 
Nimeshutushwa sana na kampuni ambayo inawakilisha Fedex Tanzania. Ukituma mzigo wowote kwa Fedex hata barua tu utasumbuliwa sana. Hawa jamaa ukituma mzigo kwa Fedex mfano hata kama mzigo ni wa $50 watajaribu kukuwekea gharama za 500,000 na zaidi.

1. Wenyewe sio TRA kodi zote zinatakiwa ziwe za TRA na sio msafirishaji cha ajabu wenyewe ndiyo wamejipa madaraka fake ya TRA.

2. Wanachelewesha mizigo makusudi kwa siku saba ili wataifishe mzigo wako na ukienda siku mzigo umefika hawawezi kukupa kwasababu wanataka wakupe storage fees.

Google review zinatisha
---

"This place turned it around in the end. I had a package shipped from US to Tanzania. There was communication in the beginning and then it stopped. We had a situation where we were traveling and needed the package before we left. We got it the day before we left but not without trials and tribulations. I'm happy that we did get our package. I'm unhappy with the timeframe and the lack of communication of SOME of the customer service agents. Would I recommend...I would never ship a package here again. BUT I did eventually get my package after being in the country 3 weeks."

"Avoid if you can even if you need to pay double to someone else like DHL. You will wait 3 times longer that with any other company because of some documents they processing extremely slow. You pay to get delivery to your address but they will call you saying that is to far so you should come to pick it up. And still they charge as per door to door. Worst experience and service from all possible international delivery companies."

"Google really need to introduce zero star rating for these kind of companies. Poor service, no response and destroying worldwide brand images. Fedex in Tanzania is one of the worst courier service you can use due to the poor service that you will encounter when your goods arrive in Tanzania."

"FedEx Tanzania is not a courier company it's a scammer and very bad treat to foreigner, they charge clearance charge more than tax amount even i did all the clearance process by other agent, also they don't deliver my goods at my place they harras me mentally and financially, I am sure one day this company will close , also they updated wrong information I went to receive my parcel myself 27th Dec but they updated 23rd December."

"I Give them One Star But to be real is Zero Star for this company. They got bad unresponsive customer service, They take too long to clear your Parcel/Package, .So Guys Don't waste Your valuable time and Money,. Choose other company !!"

Hii nchi matapeli wamejaa
 
Mkuu Kamundu hao jamaa FEDEX na DHL wote ni wezi na wababaishaji.

Wizi wao upo hapo kwenye kulazimisha kukuuzia document ya mzigo wako (airway bill) pale unapowaambia kuwa utafanya clearance wewe mwenyewe au na agent wako.

Wanasema wanakuuzia document hiyo kwa Tshs.88,000/= au la waruhusu wao wakufanyie clearance kwa Tshs. 113,000/=. Sasa unawauliza document yangu mwenyewe inakuaje niinunue?? Majibu yao ni kuwa, unainunua kwa kuwa umetumia jina lao (FEDEX au DHL). Unawaambia, si nimewalipa gharama ya kusafirisha tayari?? Baada ya hapo hujibiwi kinachoeleweka na wanasubiri siku 7 waanze kukuchaji storage

Nina imani hizi kampuni kwa Tanzania zitakuwa ni za viongozi wa siasa, ndio sababu ya kujitozea hela watakavyo na huna cha kuwafanya.

Kama alivyosema mmoja wa watoa maoni, hizo kampuni hawataki kuleta mizigo kitunda, mbezi mwisho nk kwa madai kuwa ni mbali sana, wanataka ukafuate ofisini ilhali fedha uliyolipa ilikuwa imepima umbali mpaka kwenye zipcode yako, yaani ulitakiwa ufikishiwe mlangoni kama wafanyavyo EMS au CDS.

Mimi sitaki kabisa kuwatumia hawa wezi, nawakubali sana Speedaf, hawa nawasubiri wawe na huduma nje ya aliexpress itakua poa sana
Hii inakuwaje mbona mimi nimetumiwa mzigo nikalipa online mzigo umefika?? Charges ni kawaida sasa mzigo utoke US mpaka bongo bei iwe kitoto?
 
Hii inakuwaje mbona mimi nimetumiwa mzigo nikalipa online mzigo umefika?? Charges ni kawaida sasa mzigo utoke US mpaka bongo bei iwe kitoto?
Huenda hujaelewa kinachozungumzwa, ngoja ueleweshwe mkuu.

Wewe umeagiza mzigo toka USA, umelipa labda Tshs. 50,000/= kama gharama za kusafirisha mpaka Tanzania, fedha hiyo umewalipa Fedex au DHL.

Mzigo ulipofika Tanzania, mamlaka (serikali) wanasema ni lazima ukaguliwe (clearance) ili kama unatakiwa kulipiwa kodi basi ilipwe na kama hautakiwi kulipiwa kodi basi upewe mzigo wako, hapo sasa hao Fedex wanasema kuwa uwalipe wao Tshs. 88,000/= ili wakufanyie clearance na kodi utalipa nje ya hiyo Tshs. 88,000/=. Ukiwaambia kuwa nipeni document yangu ili nifanye clearance mwenyewe, wanasema tunakuuzia document hiyo kwa Tshs. 113,000/=

Hapo sasa ndio huo tunaouita wizi!! FEDeX wanataka Tshs. 113,000/= kwa kazi gani wakati document ni zako? Unauziwaje document zako mwenyewe?? Ile elfu 50 uliyolipa si ilikuwa ni gharama ya kukusafirishia mzigo pamoja na document ya mzigo?? Kwa nini uchajiwe kwa document ambayo tayari ni yako na umeshalipia gharama za kusafirishwa kwake??

Natumai umeelewa mkuu
 
Wanakera sana,email hawajibu kwa wakati,na maswali ya kijinga mpk kuna siku wakasema niwatajie timu ya mpira ninayoshabikia,mi sio shabiki wa mpira.
Nikajibu nijuavyo wakasema nimekosea block tena.
Yaani wanafanya vitu ambavyo hawana utayari navyo.
Acc ya usd wameshindwa kuiaccess mpk leo na doc zote wanazo.🤦‍♂️
Aseeh mpk ushabiki wa timu tena
 
Huenda hujaelewa kinachozungumzwa, ngoja ueleweshwe mkuu.

Wewe umeagiza mzigo toka USA, umelipa labda Tshs. 50,000/= kama gharama za kusafirisha mpaka Tanzania, fedha hiyo umewalipa Fedex au DHL.

Mzigo ulipofika Tanzania, mamlaka (serikali) wanasema ni lazima ukaguliwe (clearance) ili kama unatakiwa kulipiwa kodi basi ilipwe na kama hautakiwi kulipiwa kodi basi upewe mzigo wako, hapo sasa hao Fedex wanasema kuwa uwalipe wao Tshs. 88,000/= ili wakufanyie clearance na kodi utalipa nje ya hiyo Tshs. 88,000/=. Ukiwaambia kuwa nipeni document yangu ili nifanye clearance mwenyewe, wanasema tunakuuzia document hiyo kwa Tshs. 113,000/=

Hapo sasa ndio huo tunaouita wizi!! FEDeX wanataka Tshs. 113,000/= kwa kazi gani wakati document ni zako? Unauziwaje document zako mwenyewe?? Ile elfu 50 uliyolipa si ilikuwa ni gharama ya kukusafirishia mzigo pamoja na document ya mzigo?? Kwa nini uchajiwe kwa document ambayo tayari ni yako na umeshalipia gharama za kusafirishwa kwake??

Natumai umeelewa mkuu
Nilichoelewa Mimi wewe mteja ndio sio muelewa kwenye meza ya watu..FedEx 88000 ni documentation (label created waybill) ni lazima uilipie ili upewe document yako ukafanye clearance Na agent wako...label created waybill haihusian Na freight charges...hii Mara nyingi utailipia kule unapoenda kupokelea mzigo wako...kwahiyo 88000 wapo sahihi mkuu...labda mengineo hapo.
 
Nimewaachia mzigo

Gharama Za kutoa ni kubwa jamani

Nikataka kutolewa na mtu mwingine .. kucollect documents wanataka 180,000 wanasema gharama ya kusafirisha documents kutoka mzigo ulipotokea [emoji119] na kule walishalipwa 200$

Na zilikua sample tu, nikaagiza nyingine zimefika na Nimepokea kwa 50$ (kila kitu included)
Nicheki tuyajenge 0689636980
 
Nilichoelewa Mimi wewe mteja ndio sio muelewa kwenye meza ya watu..FedEx 88000 ni documentation (label created waybill) ni lazima uilipie ili upewe document yako ukafanye clearance Na agent wako...label created waybill haihusian Na freight charges...hii Mara nyingi utailipia kule unapoenda kupokelea mzigo wako...kwahiyo 88000 wapo sahihi mkuu...labda mengineo hapo.
Ni sahihi mkuu. Sasa kinachoshangaza ni Cainiao kuleta mizigo yenye label hivyohivyo ila pasipo mteja kulipa chochote zaidi ya gharama ya kusafirisha.

Hata shirika la Posta tu, mtu unalipia shipping charge na sio waybill ya document yako mwenyewe, na hapo mizigo yote imekuja kwa ndege na kupita airport hiyohiyo ambayo Fedex wanataka kuchaji elfu 88. Mimi nilishajua kuwa Fedex sio mahali pangu sahihi, labda nilivamia tu, kwa hiyo nimechagua Cainiao au USPS. Napokea mzigo bila kelele
 
USPS Documentation utalipia km kawaida ingawaje charges zake ndogo mnoo..kwenye idara nyinginezo uwe vizuri mkuu..#689636980
 
Nakataa wakuu, nimesafirisha mzigo mara mbili kwa hao FEDEX na nilipokea mzigo ofisini. Rangel logistics wanajitahidi Kama una ushahidi wa tuhuma zako weka hapa ili tujifunze
 
fedex ni mwizi hawa wemeniebia mzigo wangu bataga kulipa kodi mpaka leo sizapata hasara ya laki nane
 
Nakataa wakuu, nimesafirisha mzigo mara mbili kwa hao FEDEX na nilipokea mzigo ofisini. Rangel logistics wanajitahidi Kama una ushahidi wa tuhuma zako weka hapa ili tujifunze
Na mm nilikuwa mbioni kuwatumia
 
Back
Top Bottom