DOKEZO Agent wa Fedex Tanzania (Rangel Logistics) Achunguzwe kwa kuhujumu uchumi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Utashangaa mfanyakazi wa kawaida tu wa FedEx Yuko njema, kumbe kuna uharamia unaendelea?
 
FedEx sio matapeli tatizo wabongo wanao wawakilisha fedEx hapa nchini
naamini FedEx Int'l wanaona reviews zilizopo kwenye ukurasa za hao agents pale Google na ni miaka sasa, hakuna hatua zinachukuliwa

kusema FedEx ni matapeli ni sahihi kabisa
 

Hii account ya Tanzanite ni utapeli mkubwa. Kinachotokea hata pesa zako zinakuwa hazipo wanachukuwa na kupeleka kuwekeza kwa miezi mitatu mitatu. Ukilalamika sana wanarudisha pesa.

Hii ni account maalumu kwa diaspora hivyo wanajua diaspora wengi wanaweka pesa na kuacha kwa muda mrefu wanavyofanya ukiweka pesa wana chukuwa pesa yako wananunulia CD za miezi mitatu mitatu na kupata faida kwa pesa zako wakati huohuo wanakulipisha kila mwezi na kupata dollar!!!.

Ushauri
1. Tafuta NIDA na fungua account ya kawaida
2. Acha pesa kidogo pesa nyingine peleka UTT na nunua bond fund ambayo itakulipa 12%-14% kwa mwaka. Hiyo account unatuma pesa halafu unaenda kwenye mtandao una move pesa kwenye account yako ya UTT na siku ukirudi nyumbani unakuwa na uwekezaji wa uhakika kwenye account yako badala ya utapeli wa CRDB

Mimi ndiyo niko kwenye utaratibu huu lakini usiseme unaishi nje sema uko nje kwa muda kwa shughuli zako lakini NIDA ni muhimu sana
 
UPS ndiyo mbaya zaidi ya FEDEX NA DHl combined. DHL wapo vizuri kwenye mifumo yao na wana respond haraka sana hata kabla mzigo haujafika wanakupa ulipie gharama zote. Shida ni DHL hawana shortcut. Kila kitu kinafuata utaratibu. Fedex kama unfahamiana na watu wawili au watatu utakuwa okay. Lakini UPS ni takataka kabisa usiombee mzigo uje na UPS. Bora kuliko wote ni SPEEDAF wa ALIEXPRESS. Hawa wanakuletea mzigo bure kabisa hadi mlangoni na huchajiwi sentano ya kodi, au chochote. Posta sasa hivi biashara ya vifurushi imedoda kabisa sababu SPEEDAF kateka soko lote la vifurushi kutoka China kupitia ALIEXPRESS.
 

Hii nchi matapeli wamejaa
 
Hii inakuwaje mbona mimi nimetumiwa mzigo nikalipa online mzigo umefika?? Charges ni kawaida sasa mzigo utoke US mpaka bongo bei iwe kitoto?
 
Hii inakuwaje mbona mimi nimetumiwa mzigo nikalipa online mzigo umefika?? Charges ni kawaida sasa mzigo utoke US mpaka bongo bei iwe kitoto?
Huenda hujaelewa kinachozungumzwa, ngoja ueleweshwe mkuu.

Wewe umeagiza mzigo toka USA, umelipa labda Tshs. 50,000/= kama gharama za kusafirisha mpaka Tanzania, fedha hiyo umewalipa Fedex au DHL.

Mzigo ulipofika Tanzania, mamlaka (serikali) wanasema ni lazima ukaguliwe (clearance) ili kama unatakiwa kulipiwa kodi basi ilipwe na kama hautakiwi kulipiwa kodi basi upewe mzigo wako, hapo sasa hao Fedex wanasema kuwa uwalipe wao Tshs. 88,000/= ili wakufanyie clearance na kodi utalipa nje ya hiyo Tshs. 88,000/=. Ukiwaambia kuwa nipeni document yangu ili nifanye clearance mwenyewe, wanasema tunakuuzia document hiyo kwa Tshs. 113,000/=

Hapo sasa ndio huo tunaouita wizi!! FEDeX wanataka Tshs. 113,000/= kwa kazi gani wakati document ni zako? Unauziwaje document zako mwenyewe?? Ile elfu 50 uliyolipa si ilikuwa ni gharama ya kukusafirishia mzigo pamoja na document ya mzigo?? Kwa nini uchajiwe kwa document ambayo tayari ni yako na umeshalipia gharama za kusafirishwa kwake??

Natumai umeelewa mkuu
 
Aseeh mpk ushabiki wa timu tena
 
Nilichoelewa Mimi wewe mteja ndio sio muelewa kwenye meza ya watu..FedEx 88000 ni documentation (label created waybill) ni lazima uilipie ili upewe document yako ukafanye clearance Na agent wako...label created waybill haihusian Na freight charges...hii Mara nyingi utailipia kule unapoenda kupokelea mzigo wako...kwahiyo 88000 wapo sahihi mkuu...labda mengineo hapo.
 
Nicheki tuyajenge 0689636980
 
Ni sahihi mkuu. Sasa kinachoshangaza ni Cainiao kuleta mizigo yenye label hivyohivyo ila pasipo mteja kulipa chochote zaidi ya gharama ya kusafirisha.

Hata shirika la Posta tu, mtu unalipia shipping charge na sio waybill ya document yako mwenyewe, na hapo mizigo yote imekuja kwa ndege na kupita airport hiyohiyo ambayo Fedex wanataka kuchaji elfu 88. Mimi nilishajua kuwa Fedex sio mahali pangu sahihi, labda nilivamia tu, kwa hiyo nimechagua Cainiao au USPS. Napokea mzigo bila kelele
 
USPS Documentation utalipia km kawaida ingawaje charges zake ndogo mnoo..kwenye idara nyinginezo uwe vizuri mkuu..#689636980
 
Nakataa wakuu, nimesafirisha mzigo mara mbili kwa hao FEDEX na nilipokea mzigo ofisini. Rangel logistics wanajitahidi Kama una ushahidi wa tuhuma zako weka hapa ili tujifunze
 
fedex ni mwizi hawa wemeniebia mzigo wangu bataga kulipa kodi mpaka leo sizapata hasara ya laki nane
 
Nakataa wakuu, nimesafirisha mzigo mara mbili kwa hao FEDEX na nilipokea mzigo ofisini. Rangel logistics wanajitahidi Kama una ushahidi wa tuhuma zako weka hapa ili tujifunze
Na mm nilikuwa mbioni kuwatumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…