Aggrey Mwanri: Jembe lililoachwa kimakosa kwenye Baraza la Mawaziri

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969

Kila mtanzania anamkubali Agrey Mwanri kuwa ni jembe na mchapa kazi. Anajua kuongoza, anajua kuwajibika.

Lakini kwanini kiongozi kama huyu hakupata uteuzi ili aweke mambo sawa kwa manufaa ya umma? Je, kuna tatizo kwa washauri wa rais JPM?

Mbona tuna ona watu ambao uwezo wao wa kuongoza ni mdogo na wanaingia kwenye Cabinet?

Hao wanaomshauri Rais wanakula pesa za bure za walipa kodi? Kwanini mtu kama Mwanri awe benchi, alafu watafuta kick za kwenye Tv ndio wanakula uteuzi?
 
Miaka zadi ya 65 wa nini?

Kafanya ubunge, ukuu wa mkoa na uwaziri kaleta nini?

Akiwa Tamisemi na sagi wake walikuwa wanauza ukuu wa idara kwa sh ngp?
Wewe ni mpumbavu.
 
jiwe huwa ana reserve yake, amini kwamba haitopita miaka 2 kuanzia sasa hajawarudisha hawa
1. Makonda
2. Mwanri
3. Kigwa
 
Mzee wa Toronto

Tabora wanammisi sana mzee na mbwembwe zake.

Ila tamaa mbaya
 
Alifanya nini zaidi ya kiki na masihara. Kwanza alistaafu kwahivyo mwacheni apumzike nchi inavijana wengi tuu wasomi na wawajibikaji waliokosa kazi
 
Comedy zake zimemponza
 
Mwanri Huyu huyu aliyesema inabidi Mungu amshukuru Magufuli ?
Huyu huyu ambaye hakuwa akichuja mawazo yake kabla ya kuyatamka, anayetoa macho kama mzee wa mofaya na kupenda misifa ?

Tafsiri/maana ya kiongozi mzuri/bora na mtendaji mzuri mnaichukulia referencence kwa jiwe ?
 
Kila mtanzania anamkubali Agrey Mwanri kuwa ni jembe na mchapa kazi.

Anajua kuongoza, anajua kuwajibika.
Aggrey Mwanri hana lolote zaidi ya UROPOKAJI na Komedi za kwenye TV. Kiukweli SIYO MTENFAJI ndiyo maana silaha yake kubwa ya kuonwa na mabosi wake ni KELELE tu.
 
Mimi binafsi namuona mzee msanii tu.
 
nilikuwa namkubali sana kipindi yupo tamisemi... alikuwa anaijua mitaa na vijiji vyote na nilikuwa nampenda sana alivyokuwa anajibu maswali bungeni ila huku kwenye ukuu wa mkoa sifa zilikuwa nyingi sana.... baada ya kupata promo kwenye public akataka kwenda na upepo huo huo
 
Hili jembe halikustahili kukaa benchi as state funny man and hard worker he deserves achance
 
Na Makonda ni nani Fyekeo eti?
 
Mwanri ni mzalendo wa kwrli, na ana hofu ya Mungu. Issue kubwa ni kwamba sio wa Kanda ya Jiwe..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…