KERO Agha Khan Hospital Iringa huduma zenu ni mbovu sana

KERO Agha Khan Hospital Iringa huduma zenu ni mbovu sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Tony Yeyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Posts
733
Reaction score
570
Ninapenda kutoa malalamiko kuhusu huduma duni niliyoshuhudia katika Hospitali ya Aga Khan Iringa.

Nilimpeleka mke wangu siku ya Jumamosi majira ya saa 10:30 jioni. Tulipofika, tulikuta dada wa mapokezi akiondoka bila kutoa maelezo yoyote kwa wagonjwa waliokuwa wakisubiri.

Cha kushangaza, alienda kukaa pembeni akizungumza na rafiki yake huku wagonjwa wakibaki bila msaada, wakijiuliza nini cha kufanya.

Wagonjwa wanapokuja hospitalini, wanahitaji huduma ya haraka, maelekezo ya wazi, na kuhudumiwa kwa heshima. Ni vyema mjitathmini na mjirekebishe ili kutoa huduma bora kwa kila mgonjwa bila upendeleo wala uzembe.

Tafadhali chukueni hatua. Huduma za afya si mahali pa mzaha.
 
Hospital ya Agha kan iringa huduma zenu mbovu, nilimpeleka wife siku ya jumamosi mida ya saa kumi na nusu jion , dada wa mapokezi katoka ameacha wagonjwa akaenda kutia Stori na ya rafiki yake bila ata kutoa Maelezo yoyote
Wagonjwa wakabak waanaulizana maswali bila msaada wowote, jifunzen kutoa huduma bora kwa wagonjwa

Hii sio Sawa jirekebishen
Unajua ukiwa na passion na kazi unajituma kwa kazi kwa moyo na unafuata ""ETHICS ZA KAZI ""

MBONA WENGINE TUMEJALIWA MOYO WA UPENDO KUJITUMA NA KWA BIDII KUBWA SANAAAAAA BROTHER NA TUNAFANYA KAZI KWA UZALENDO MKUBWA SANAAA

Mara KADHAA nime wai kuweka wazi kua Mimi ni mdau wa afya mwandamizi senior Mimi vipimo vyotee vipo nyumbani eg. Mrdt, multstick, HIV TEST, BP mashine, stestescope e.t.s Ila mwanangu mdogo aliugua Ila wife haniamini Mimi kumpima mtoto akampeleka private hospitals moja yaan wakipewa HUDUMA mbovu kwa kiwango Cha SGR.

Unajua hata mkiwa na mtaalamu wa Sheria ama engineer ama hata dactari , mwalimu, muhasibu, mfano mama yake Magufuri aliwai kusema mwanae hawezi kua Raisi wa kuongoza bukoba mpaka mtwara haahaa kwa Sasa wife kaanza kua na Imani na Mimi. ☺️🤓

Kazi ni passion na moyo wa kazi mfano Kuna ma barmaid Wana enjoy kazi zaooo
 
Back
Top Bottom