Agizo la Rais juu ya taasisi za Serikali kupewa kazi za ushauri liliishia wapi?

Agizo la Rais juu ya taasisi za Serikali kupewa kazi za ushauri liliishia wapi?

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,319
Reaction score
3,128
Rais anaposonga mbele, aliyoagiza nyuma yanasahaulika. Muongozo ulitolewa na serikali ya awamu hii ikiwa ni pamoja na ofisi za serikali kuhamia majumba ya serikali, mikutano kufanyika nyumba za serikali, kazi za ushauri kufanywa na taasisi za serikakali. Nionacho ni mapambano kati ya tabia za watendaji na rais wa nchi.

Nimetembelea Ofisi za Open University (OUT) mjini Morogoro, ziko vichocholoni zaidi ya kilomita 10 kutoka mjini, kwenye nyumba ya mtu binafsi. Kwa nini walihama nyumba ya serikali, katikati ya mji, haieleweki. Walipo sasa hivi ni mateso kwa wahitaji huduma.

Wizara na taasisi za serikali pia kwa sasa wanatoa kazi za ushuri wa kitaalamu (Consultancies) kwa watu binafsi na siyo taasisi za serikali kama walivyotuaminisha wakati awamu ya 5 inaingia madarakani. Ubora wa kazi ni mbaya sana lakini wanaendelea kufanya hivyo.

Hawana sababu zaidi ya 10% ambayo wanashindwa kuipata wanapotumia taasisi za umma. Je, Vita hii ya rushwa na ufisadi itafanikiwa?
 
Mapambano ya ufisadi ni ubunifu wa rais tu. Mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi, na wote ndani ya ofisi za serikali bado wanahitaji rushwa na ufisadi sana!

Kazi za ushauri, bado ni shida hata kwa makampuni binafsi. Maofisa wakitangaza kazi hizo, wanakupigia simu wakiuliza utawapa ngapi, bila kujali uwezo unao au hapana. Lengo siyo ushauri, ni pesa. Mfano mzuri angalia taarifa za wizara ya maji na miradi yao.
 
Back
Top Bottom