Agizo la Rais Magufuli la mashirika yasiyotoa gawio kwa Serikali latekelezwa ndani ya saa 24

Agizo la Rais Magufuli la mashirika yasiyotoa gawio kwa Serikali latekelezwa ndani ya saa 24

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
461
Reaction score
295
1574747212865.png

Saa chache baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa siku 60 kwa Taasisi, Kampuni ambazo Serikali ina hisa chache na Mashirika ya Umma 187 ambayo hayajatoa gawio au mchango kwa Serikali tayari Taasisi nne zimetekeleza agizo hilo leo.

Akizungumza leo, jijini Dodoma, wakati akipokea gawio na michango kutoka Shirika la Posta, Shirika la Reli (TRC), Self Microfinance Fund, na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ambapo jumla ya fedha zilizowasilishwa ni shilingi bilioni 2.75, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema kuwa baada ya agizo la Rais alilolitoa jana, hakutakuwa na mzaha kwa Taasisi, Kampuni na Mashirika ambayo hayatekeleza agizo hilo ndani ya siku 59 zilizobaki.

“Nitasimamia kikamilifu agizo hili la Mheshimiwa Rais, itakapofika siku ya 60 nitatembeza panga bila uoga wala kupepesa macho kwa Taasisi, Kampuni na Mashirika ambayo hayatakuwa yametekeleza agizo hili, hatutanii katika hili” alisema Waziri Mipango.

Aidha, Waziri Mpango alizishukuru Taasisi hizo kwa kutekeleza agizo la Rais na kuongeza kuwa angependa kuona Mashirika yaliyobaki yakitekeleza agizo hilo kwa wakati, kwa kuwa fedha hizi si zake wala za Rais bali ni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa faida ya watanzania wote.

Naye, Msajili wa Hazina, Athumani Mbutuka alisema kuwa alitekeleza agizo la Rais Magufuli la kumtaka kuzijulisha Taasisi, Kampuni na Mashirika 187 ambayo hayakuwa yametoa gawio na michango kufanya hivyo ndani ya siku 60, ambapo Taasisi za TRC, TIC, Shirika la Posta na Self Microfinance Fund wamekuwa wa kwanza kutekeleza agizo hilo.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana alipokea gawio na michango kutoka kwa Taasisi, Kampuni na Mashirika 79 ambayo yalitoa jumla ya shilingi trilioni 1.05, ambapo Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro, Wakala wa Huduma za Misitu na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) yalikabidhiwa cheti kwa kufanya vizuri. Aidha, TPA iliyotoa gawio la shilingi bilioni 169 na TPC iliyotoa shilingi bilioni 14 yalipewa tuzo kwa kutoa gawio kubwa zaidi.
 
Hakuna mtu au kiongozi nchini anayependa kuachishwa/kuacha nafasi yake ya kazi.

Kuna viongozi wengine wataenda hata kukopa ili tu waonekane wametoa gawio kwa serikali!

Duh! Rais Magufuli anawapa baadhi ya watu/viongozi magonjwa ya moyo!
 
Hakuna mtu au kiongozi nchini anayependa kuachishwa/kuacha nafasi yake ya kazi.

Kuna viongozi wengine wataenda hata kukopa ili tu waonekane wametoa gawio kwa serikali!

Sio kuachishwa tu, na kutiwa doa kwenye CV yako pia. Watauza hata nyumba zao wengine!
 
Tunategemea mapato yatakuwa zaidi ya trilioni mbili kwani mashirika yaliyobaki ni mengi zaidi
 
Hakuna mtu au kiongozi nchini anayependa kuachishwa/kuacha nafasi yake ya kazi.

Kuna viongozi wengine wataenda hata kukopa ili tu waonekane wametoa gawio kwa serikali!
Ni sawa hata wakikopa. Ili next time waongeze juhudi ya kutafuta mapato. Kuna taasisi toka zimeanzishwa hazijawahi kutoa gawiwo kwa Serikali. Lakini kila siku wanapandisha mishahara na posho.
 
Hizi taasisi za magawio watupatie mahesabu yao wazi (zinaeza kuwa ziko na open access ) ila watuonyeshe tu wazi wazi sambamba na magawio yao, tuangalie hizo devidends na ROI na RE
 
Tunategemea mapato yatakuwa zaidi ya trilioni mbili kwani mashirika yaliyobaki ni mengi zaidi
Kumbuka mheshimiwa alisema hao wasioleta gawio najua wapo guest house unadhani watakuwa wamebaki na sh ngapi ? Mimi naona kama wameamka ghafla wamekuja na taulo wakirudi ofisini wataleta gawio LA kueleweka
 
Kumbuka mheshimiwa alisema hao wasioleta gawio najua wapo guest house unadhani watakuwa wamebaki na sh ngapi kwa staili hii ya Kukurupushwa? Mimi naona kama wameamka ghafla wamekuja na taulo nadhani wakirudi ofisini wataleta gawio LA kueleweka
 
Hakuna mtu au kiongozi nchini anayependa kuachishwa/kuacha nafasi yake ya kazi.

Kuna viongozi wengine wataenda hata kukopa ili tu waonekane wametoa gawio kwa serikali!

Duh! Rais Magufuli anawapa baadhi ya watu/viongozi magonjwa ya moyo!
Haya ni majibu ya wazi kuwa ANADANGANYWA SANA na ma CEO wa taasisi mbalimbali.
Zilikuwa wapi hizo pesa? Zimepatikana wapi hizo pesa? Sasa nimeamini ile habari kuwa kuna watumishi wa umma wanaweza kuhamisha fedha za miradi ambayo wanajua utekelezaji wake uko mbali may be more than six month kwenda kwenye bank za biashara na kufungulia account maalum ya faida, fixed deposit a/c kwa makubaliano maalum.
Sasa mfano imewekwa Bill 3 kwa 9% tuu miezi 6 jamaa wanavuta karibu 270m za bure.
Ulaji umebadilishiwa njia tuu
 
Tunategemea mapato yatakuwa zaidi ya trilioni mbili kwani mashirika yaliyobaki ni mengi zaidi
Alafu hayo mashirika yataenda kuomba ruzuku ili yaweze kujiendesha, hivyo yatarudishiwa pesa walizotoa au zaidi, hivyo serikali italazimika tena kukopa kuyafadhili hayo mashirika.

Vituko.
 
Hivi kanuni ya kufahamu gawio kutoka hizi taasisi ikoje na hutolewa kila baada ya muda gani?Tufahamisheni Sisi tusiofahamu.Je,miaka ya nyuma vipi?
 
Back
Top Bottom