Agizo la Waziri Silaa la kuhamishia Huduma za Ardhi ofisini kwake laanza kutekelezwa Dodoma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Mamia ya wananchi wamemiminika katika viwanja vya Ofisi za Halmashauri ya jiji la Dodoma kutatua madhila ya ardhi yanayowakabili ili watumie ardhi na muda wao kwa shughuli za kiuchumi kujiletea maendeleo.

Akizungumzia zoezi hilo linaloendelea jijini Dodoma, Katherine Mwimbe Mwekezaji na Mkurugenzi wa Taasisi ya Domaiya Estate Dodoma Tanzania inayojishughulisha na usindikaji wa mvinyo na huduma za hoteli ni miongoni mwa waliopata huduma kwenye Kliniki ya Ardhi inayoendelea jijini Dodoma ambapo amesema ameridhishwa na huduma zinazotolewa katika zoezi hilo.

“Tumekuwa na changamoto za ardhi katika uwekezaji wetu, tumepata simu tukakaribishwa katika kambi hii maalum inayozungumzia masuala ya ardhi, tuliambiwa tufike saa 2:30, tumefika kwa wakati mara moja tumepata huduma tunayohitaji, tumekuja na nyaraka zetu. Vitu vimefanyiwa kazi, tunapata matumaini na tuanweza kuendelea na uwekezaji na biashara” amesema Mwimbe.

Mwimbe ameongeza “Sisi kama kampuni ya kimataifa tumepata huduma nzuri, hiyo imetupan sana moyo, naamini tunaweza kwenda kufanya maendeleo zaidi hasa katika sekta ya mvinyo hapa Dodoma.

Zoezi hilo linaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga, Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera, Kamishna wa Ardhi Methew Nhonge, watendaji wa wizara hiyo pamoja na watendaji wa Ardhi mkoa wa Dodoma.

========

Snapinsta.app_445169857_18317764606183394_36143985446128926_n_1080.jpg

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa (Kulia) akifunga kufuli kwenye ofisi ya Masijala ya Ardhi ya jiji la Dodoma alipokwenda kuzifunga rasmi ofisi hizo tarehe 28 Mei 2024.

Snapinsta.app_444216171_18317764603183394_5691767685660801443_n_1080 (1).jpg

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa (Kulia) akimkabidhi fungua Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga mara baada ya kuzifunga ofisi ya Masijala ya Ardhi ya jiji la Dodoma, Mei 28, 2024.​
 
Mamia ya wananchi wamemiminika katika viwanja vya Ofisi za Halmashauri ya jiji la Dodoma kutatua madhila ya ardhi yanayowakabili ili watumie ardhi na muda wao kwa shughuli za kiuchumi kujiletea maendeleo.

Akizungumzia zoezi hilo linaloendelea jijini Dodoma, Katherine Mwimbe Mwekezaji na Mkurugenzi wa Taasisi ya Domaiya Estate Dodoma Tanzania inayojishughulisha na usindikaji wa mvinyo na huduma za hoteli ni miongoni mwa waliopata huduma kwenye Kliniki ya Ardhi inayoendelea jijini Dodoma ambapo amesema ameridhishwa na huduma zinazotolewa katika zoezi hilo.

“Tumekuwa na changamoto za ardhi katika uwekezaji wetu, tumepata simu tukakaribishwa katika kambi hii maalum inayozungumzia masuala ya ardhi, tuliambiwa tufike saa 2:30, tumefika kwa wakati mara moja tumepata huduma tunayohitaji, tumekuja na nyaraka zetu. Vitu vimefanyiwa kazi, tunapata matumaini na tuanweza kuendelea na uwekezaji na biashara” amesema Mwimbe.

Mwimbe ameongeza “Sisi kama kampuni ya kimataifa tumepata huduma nzuri, hiyo imetupan sana moyo, naamini tunaweza kwenda kufanya maendeleo zaidi hasa katika sekta ya mvinyo hapa Dodoma.

Zoezi hilo linaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga, Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera, Kamishna wa Ardhi Methew Nhonge, watendaji wa wizara hiyo pamoja na watendaji wa Ardhi mkoa wa Dodoma.
Asante Waziri , Slaa.
 
Akija waziri mwingine anakuja na mpango kazi wake wa hovyo kizungumkuti!
 
Back
Top Bottom