TANZIA Agnes Nasania Diwani Kata ya Shelui, Wilaya ya Iramba afariki Dunia

TANZIA Agnes Nasania Diwani Kata ya Shelui, Wilaya ya Iramba afariki Dunia

Ni mpumbavu pekee anayeweza kushiriki kumwua mwanadamu mwenzake kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa yeye mwenyewe kufyatua risasi, kutoa amri ya kuua au kushabikia na kuunga mkono mauaji kwa sababu tu ya madaraka, akiamini kuwa ameshinda au akiamini amemwadhibu au kumkomoa aliyeuawa, wakati na yeye, hata kama siyo kwa risasi, lakini yupo safarini kuelekea kufa.


Watawala, waliotoa amri ya kuua, polisi walioua, TISS wanaoteka na kuua na CCM inayosimamia sera za mauaji, wote wamenyimwa hekima, madaraka yamewapumbaza, na kujiona wao ni waamuzi wa nani aishi na nane afe. Mungu anapomchukua mmojawao anawakumbusha kuwa hata wao wapo safarini kukielekea kifo. Je, wangapi wanalielewa hilo? Au ndiyo wamenyimwa ufahamu, na kufanywa vipofu wa akili na macho?

Marehemu Agmes na familia yake hatujui kwa uhakika mioyo na matendo yao yalikuwa vipi, na kwa sababu hatujui, na kwa kuwa nasi ni wanadamu, na kwa sababu ni mwanadamu mwenzetu, tunaipa familia yake pole nyingi, na kumwombea Agnes kwa Mungu ampe pumziko jema. Ameimaliza safari yake hapa Duniani, mengine ni Muumba wetu ndiye ajuaye na ndiye muamuzi.

Tuliobakia ndio tunatakiwa kujifunza.

Tuombe sana hekima ya Mungu, maana mtu unaweza kuhangaika sana, unaweza kuhonga, unaweza kuwaua wanadamu wenzako, na baadaye kweli ukayapata madaraka, halafu baada ya miezi, mwaka mmoja au miwili, hupo tena Duniani. Nina hakika laiti ungejua usingejihangaisha na madaraka ya Duniani, zaidi ungejitahidi kuyatengeneza maisha yako ya milele ili uwe na nafasi katika ufalme wa Baba wa mbinguni, ungejitahidi kuitafuta hekima ya kumfahamu Kristo Yesu, aliye njia pekee ya kumfikia Baba na mfalme wa mbingu.

Wauaji wote na mnaoshiriki mauaji kwa namna mbalimbali, mwelekeeni Baba wa mbinguni, mkayajutie maovu yenu, ili kuitafuta huruma ya Mungu. Hakika nawaambieni wauaji wote, mliwaua watu wengi mkiamini mtayatwaa madaraka, na mkishayatwaa mtayafurahia, lakini nawaambieni, kwa hakika kamwe hamtayafurahia madaraka mliyoyanunua kwa damu za watu, badala yake mtabakia kujutia wakati wote. Tume bandia kamwe hazitawapeni furani yoyote, badala yake zitazidisha mateso ya mioyo yenu.
 
Jina lake hilohilo
Agnes hapa JF ni hawa
Screenshot 2026-05-31 at 19.10.31.png
 
Wakuu nasikitika kutangaza kifo cha diwani huyo na mwana JF mwenzetu.

Diwani Kata ya Shelui, Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida kupitia chama Cha Mapinduzi CCM, Agnes Nasania Amos amefariki dunia ghafla.

Mwenyekiti wa Halmashauri Innocent Msengi, Baraza la Madiwani, Menejimenti na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wametoa pole kwa Ndugu, Jamaa na Watanzania wote kufuatia msiba huo.

Kwanini anaonesha manyonyo? Na kwa nini alikuwa ccm?
 
Wakuu nasikitika kutangaza kifo cha diwani huyo na mwana JF mwenzetu.

Diwani Kata ya Shelui, Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida kupitia chama Cha Mapinduzi CCM, Agnes Nasania Amos amefariki dunia ghafla.

Mwenyekiti wa Halmashauri Innocent Msengi, Baraza la Madiwani, Menejimenti na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wametoa pole kwa Ndugu, Jamaa na Watanzania wote kufuatia msiba huo.

Nono yake nyeupe
 
Back
Top Bottom