OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 457
- 773
Maskini hutapeliwa zaidi na hii ni sababu kubwa, weka laki moja baada ya miezi mitatu utarudishiwa laki tatu
Utapeli kimsingi upo tangu enzi na kila mtu anaweza kutapeliwa kwa namna moja au nyingine
James Randi alisema, No matter how smart or educated you are, you can easily be deceived. So no one escapes utapeli
Ila linapokuja swala la kutapeliwa hasa pesa, masikini wanakuwa katika hali ya kutapeliwa kirahisi sana. Tuelewe kihesabu, tajiri anaweza kutapeliwa kiasi kikubwa, lakini kiasi kikubwa cha tajiri ukifananisha na amali zake unakuta ni kidogo. Lakini masikini unaweza kumkombeleza kabisa
Iko hivi, katika biashara mtu hupaswa kuangalia profile au muenendo wa biashara husika wa jinsi ambavyo itafanyika kujua hatari na vitu vingine kama hivyo kabla ya mtu kuwekeza katika baisahara husika
Hali imekuwa tofauti kwa masikini waliowengi ambao wao huangalia faida tu, sasa matapeli wa kisayansi wanakuja na biashara zao na kuwaambai watu wawekeze kwa maneno kuwa watapata faida ya 100% baada ya muda fulani i,e DECI, hawa watu bila kufikiria namna ambavyo biashara hiyo itafanyika huweka pesa, na siku ya gawio wanaambiwa kuwa biashara haikufanya vizuri hivyo hakuna gawio wala kurudishiwa hela waliowekeza
Kwa hiyo utaona utaona masikini wengi hutapeliwa kwa ahadi ya faida kubwa ambayo inawafanya wachanganyikiwe na kuwekeza bila kuangalia risks zinazowezakujitokeza, najua mnajua kuhusu paratuparatu/kekundu na michezo mingine ambayo inayoahidi mara mbili ya hela unayoweka
Sasa jiulize unadhani matajiri wa Tanzania waliuingia mtego wa DECI au mitego mingine mingi inayoendelea kuwepo? Ni kwa sababu akili zao hazipo kwa faida peke yake bali namna faida husika inaweza kufikiwa
USHAURI
Acha tamaa, hata kama kitu kinakuonyesha faida kubwa, jaribu kudadisi kujua jinsi faida unayoahidiwa inaweza kufikiwa, Hii ni kwa maswala ya uwekezaji. Sizungumzii gambling kwa kuwa they are just chances
Ukitaka kuwekeza kwenye hisa au biashara za kifedha, jaribu kusoma kuhusu namna kampuni inaendesha pia tafuta finacia and income statements ili kuona usalama wa uwekezaji wako
Kigezo chako cha kuwekeza kisiwe faida bali namna ambayo hela ndogo utakayoiweka haitapotea
Signed
Oedipus