Juma Wage
Senior Member
- Sep 8, 2023
- 132
- 279
Katika vitabu vya historia ya siasa, kuna sura ambazo huandikwa kwa wino wa aibu na masikitiko. Hii ni moja ya hizo. Ni simulizi ya mwanasiasa aliyejivika joho la mkombozi, akawaahidi wanachama wa CCM Kawe “miujiza” ya maendeleo, lakini akawatelekeza katikati ya ahadi hizo.
Josephat Gwajima, akitokea kwa kishindo kama mvuvi wa roho, aliingia Kawe kwa maneno matamu na ahadi za kuvutia kuwa kila kata itapata ofisi mpya ya CCM ya ghorofa.
Akawaaminisha, akawasukuma, wakavunja ofisi zao za zamani alizozikuta zikibeba historia ya chama na jasho la wazee waliopigania rangi ya kijani.
Akapeleka matrekta, akaangusha kila paa, kila ukuta kwa ndoto ya kisasa iliyojengwa kwa hewa.
Lakini ndoto hiyo iligeuka mzimu. Ofisi mbili tu ndizo zilizoanza kujengwa, nazo zimeishia usawa wa madirisha, zikiwa kama sanamu za mashaka.
Kata nyingine zimebaki na mawe ya ahadi, na CCM Kawe sasa inafanya shughuli zake katika ofisi za kukodi, jambo linalowafanya wanachama wajisikie kama wapangaji ndani ya nyumba yao wenyewe.
Hasira zimefika kileleni. Gwajima sasa anaitwa “Kibwetere wa Kawe,” jina lenye kumbukumbu ya udanganyifu wa kiimani, lililojaa hila, tamaa na usaliti.
Wanachama wanahoji: Je, hii ndiyo CCM aliyoiombea kura? Je, hii ndiyo dhamira ya ujenzi wa chama, au ni jukwaa la maigizo ya kisiasa?
Simulizi hii ya Kawe inabaki funzo kuwa si kila anayetoa ahadi ni mjenzi, na si kila mnara wa maneno huzalisha matofali.
Chama kinahitaji viongozi wenye uaminifu, si wasanii wa ndoto.
Alamsiki!