Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Leo Jumatano, Desemba 11, 2024, mapema katika kuendeleza hamasa za klabu ya Simba kuelekea mchezo dhidi ya CS Sfaxien ya nchini Tunisia, Jumapili Desemba 15, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally, akiwa katika maeneo ya Tandika, tawi la Kapu la Magori, alitoa dongo kwa Yanga kwa kuifananisha na Simba B.
Soma, Pia: Beki wa zamani wa Simba SC, Israel Mwenda atua Yanga kwa Mkopo akitokea Singida Big Stars
Kauli hiyo inakuja baada ya saa chache watani zao, kukamilisha usajili wa mkopo wa miezi sita (6) wa beki Israel Patrick Mwenda akitokea Singida Big Stars na kukamilisha idadi ya nyota wanne ndani ya kikosi cha Yanga ambao waliwahi kuitumikia Simba SC.
Nyota hao ni: Jonas Mkude, Clatous Chama, Jean Baleke na Israel Mwenda