Ahmed Ally: Tarehe 19 tunacheza na timu kubwa iliyotuzidi makombe 8.

Yanga ni yangapi kwenye rank za CAF kwasababu simba ni ya 7 na ilishawahi kuwa ya 5,na timu kubwa na bora zipo kwenye rank za CAF
 
Ahmed Ally amesema Ukweli kabisa, Simba tunatakiwa tujipange sana ili kushinda au kutoa sare na Yanga kwakweli

Kuhusu kuchukua makombe mengi ni kweli Yanga wametuzidi kwa kuwa na Makombe mengi lakini watafungika tu tukiweka kikosi kizuri
 
Tuna nafasi ya kushinda, lakini tujiandae na kuomba sana Mungu....max zengeli nahisi atafunga hii game
Nadhani Simba wataingia kwa kucheza mpira wa kasi kwa dakika 15 za mwanzo ili wapate goli la mapema kuwavuruga wachezaji wa Yanga. Kama Yanga ikiweza kuhimili presha za dakika 30 za kwanza basi watakuwa wame uwin mchezo na mbinu za Simba.
 
hakuna cha kujifariji wala nini kipga kitakatifu na kikubwa zaidi kinawahusu hawa mbumbumbu!
 
“Tarehe 19 tunaenda kucheza mechi na mkubwa wetu ambae ametuzidi mwaka mmoja wa kuzaliwa na anatuzidi makombe[emoji471][emoji966] nane 8 ya ligi, hii ni mechi ambayo inabeba taswira ya soka letu la tanzania.
Wapi kayasema hayo ?Leta Ushahidi hapa tuone siyo hizi mpyompyo zako.
 
Huyu jamaa wa Kaole sanaa group Ahmed Ally anajaribu kuipumbaza Yanga ivimbe kichwa na kunyanyua mabega kuwa ni bora kuliko Simba ili ifungike kirahisi mbinu ya kizamani enzi za mwalimu!!

Yanga sio wajinga wanajua ubingwa wao hutoka kwenye points sita za simba hivyo Yanga itacheza kufia uwanjani. Ukisikiliza interview ya Kibabage kasema hawaidharau simba hivyo Kipigo kiko pale pale!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…