The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa Simba ni miongoni mwa timu zinazotoa vipigo vikubwa barani Afrika huku akisisitiza kuwa tayari wamewahi kuwadhalilisha wapinzani wengi, ikiwa ni pamoja na Horoya AC.
Hata hivyo, anasema hawajawahi kufanya hivyo kwa timu kutoka Uarabuni jambo analodai litabadilika, kwani kwa sasa ni zamu ya Al Masry kupokea kichapo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Ahmed amesema ushindi huo utakuwa mfano kwa timu nyingine barani Afrika.
Akizungumzia mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC), Ahmed amebainisha kuwa mabao mawili waliyofungwa nchini Misri si changamoto kubwa na anaamini yanaweza kulipwa kipindi cha kwanza tu. Ametoa kauli hiyo kwa kujiamini, akieleza kuwa Simba tayari imepita vizingiti vigumu na sasa haina hofu ya kwenda kufanya makubwa katika mchezo huo wa Aprili 9, 2025 na kutinga hatua ya nusu fainali.