Ahmed Ally: Tumezidiwa na Yanga

Ahmed Ally: Tumezidiwa na Yanga

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
22,719
Reaction score
40,739
Baada ya kipigo cha 5-1 kutoka kwa Yanga, Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema "leo tumezidiwa na mpinzani wetu na hatimaye tumeadhibiwa, hakuna unachoweza kusema zaidi kukiri udhaifu kwa upande wetu.

Hili limepita japo linaumiza na haliwezi kufutika katika mioyo yetu lakini muhimu ni kuganga yajayo."

Ametoa rai kwa klabu hiyo kutopoteza umakini akisema "tumepoteza mechi moja bado tuna mechi nyingine mbele za kupigania malengo yetu."
 
Basi sawa!
Tumekusikia semaji la CAF!!
 

Attachments

  • VID-20231105-WA0025.mp4
    3.4 MB
Kukili makosa na kutoyarekebisha ni upumbavu wa hali ya juu.For how long have we been complaining about the quality of our coach?mnaleta ngonjera tu hapa mara pira kokoto,mara mpira sijui majivu sijui objenini bumbavuuuuuu!
Na kikosi pia ni cha kutazamwa. Hakuna rotation.
Saidoo, Chama, kapombe, Inonga, Kanute, mzamiru kila mechi wanacheza wao tu. AFL, ligi ya mabingwa, mechi za ndani. Wengine umri ushaenda kwanini wasichoke? Kuna siku tutapigwa 8 au 10 tukikotana na timu aggressive enough.
 
Huu udhaifu mbona wa muda mrefu tangu ligi imeanza. Je viongozi na benchi la ufundi walichukua hatua gani. Ukirudi nyuma tu kidogo uaktizama mechi mbili na wazambia na zile mechi mbili za Al AHLY utaona kabisa kuwa kuna jambo baya litAkuja kutokea mbele ya safari na la kushukuru Mungu tu timu ilikuwa na bahati kuepuka vipgigo vya aibu mpalka leo ilipokumbana na dhahama.

Na lilikuwa kosa kubwa la kiufundi kwa benchi la ufundi la Simba kuamua kupishana na Yanga yenye kasi na stamina kuliko wao Simba. Benchi la ufundi la Simba leo walitakiwa wasione aibu wangepaki basi mwanzo mwisho wawachie Yanga wacheze na wao kushambulia kwa kushtukiza lakini wao walikuwa hawajui madhaifu ya timu yao kwenye stamina na kasi wakajichanganya kuanza kupishana na Yanga na hapo ndio kipigo kilipoanzia.
 
Back
Top Bottom