Ahmed Kombo: Waziri Katambi kitendo cha kufungia mikutano ya siasa, mimi nakutafutia zawadi ya mbuzi

Ahmed Kombo: Waziri Katambi kitendo cha kufungia mikutano ya siasa, mimi nakutafutia zawadi ya mbuzi

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Mwanaharakati Ahmed Kombo, ameahidi kutoa zawadi ya Mbuzi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ikiwa ni pongezi baada ya hatua ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa

"Waziri kitendo cha kufungia mikutano ya siasa, mimi nakutafutia zawadi ya mbuzi. Niko tayari kukabidhi zawadi ya mbuzi siku yoyote niite. Maana mimi ni mfugaji wa mbuzi. Nitakukabidhi zawadi ya mbuzi, mbuzi... mbuzi kweli kweli.

Natangaza zawadi ya kumkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani, zawadi ya mbuzi kwa kuzuia mikutano ya kisiasa kwenye taifa hili.

Hata Dkt. John Pombe Magufuli alifanya hili zoezi, alizuia mikutano, alizima live za Bunge. Kwa sababu gani? Aliona siasa wanayoifanya wapinzani haina afya. Ni siasa ya chuki. Ushanifahamu eh? Ni siasa ya chuki, ndio maana akapiga block, akapiga 'tii'



 
CCM NI WAPUMBAVU SANA MKUU, LAKINI NITAKUJIBU KWA KIFUPI ANAEVUNJA UTULIVU/AMANI NI....

1. Anayeteka watanzania Wenzetu akina Soka, Polepole, Mdude, Chaula nk.

2. Anayepiga watu Risasi Akina TUNDU LISSU, SATIVA AKWILINA MAWAZO NK

3. Anayezuia haki ya Kikatiba ya Mikitano ya Vyama vya siasa.
(Kushiriki mikutano ya hadhara na Mikutano ya ndani.

4. Anayezuia Maandamano ambayo ni haki ya kikatiba ya Tanzania.

5. Anayezuia na Kupora Haki ya watanganyika ya kuchagua kiongozi wanaye mtaka.

6.Anayeficha Kila aina ya mikataba, Bandari, Ardhi, Dhahabu, Gesi nk.

7. Anayekandamiza uhuru wa vyombo vya Habari

CCM WAMETUONA WATANGANYIKA NI MALOFA SANA


AMKENI WATANGANYIKAb
 
Mada takataka za watu wenye uwendawazimi kama huyo sijui Kombo, msiwe mnaleta JF, zinajaza sefver bure.
 
Back
Top Bottom