Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
AHMED MOHAMED JOHARI (MNUBI) YANGA WALIMKATISHA MASOMO SEKONDARI ACHEZE MPIRA
Picha hiyo hapo chini inatoka kwa Sunday "Computer'' Manara na yeye kaipata kwa kaka yake Kitwana ''Popat'' Manara.
Caption ya picha ni kutoka kwake Sunday:
''Waliosimama/kuanzia kushoto, Golikipa- Haji Masajage, Abasi Khalid, Jamil Hizam, Hassan Goboss, Kitenge Baraka, Jina limenitoka, anae fuatia Boi Wickens, Omari Kapera, Shabani Jangama, Semboko.
Chuchumaa- jina sina anaefuata ni Brayan Sagatwa, Maulidi Dilunga, Mohamed Msomali, Abdul Rahman Juma (Capt), Kilambo Athumani na Mnubi.
Picha hii kwa hisani ya Kitwana Manara ni ya muda mrefu.''
Katika picha hiyo wengi nilifahamiananao lakini napenda kumzjungumza Mnubi kwani yeye tulijuana tukiwa wadogo shule ya msingi:
''Mimi niliingia shule ya Kinondoni darasa la tano mwaka wa 1963 nikitokea Majengo Middle School Moshi nikamkuta Mnubi yuko darasa la sita.
Sote tulikuwa watoto wa Gerezani na tukicheza mpira pamoja Kidongo Chekundu lakini Mnubi kwa umri alinipita sana kwa hiyo sikupata kucheza na yeye kiwanja kimoja.
Mnubi alikuwa na sifa kubwa mbili.
Alikuwa hodari darasani na akijua sana mpira.
Alikuwa mrefu wa sifa na mweusi sana kama Wanubi walivyo mwangalie hapo chini kwenye picha.
Mwalimu Mkuu wa shule yetu Mr. Reveta akimpenda sana.
Mimi asubuhi nikimpitia Mnubi kwao Mtaa wa Kiriki (Kirk Street) tukiongozana kwenda shule na tukirudi pamoja.
Nyumba yao ilikuwa ubavu kwa ubavu na nyumba ya Bi. Mruguru bint Mussa mama yao Abdul, Ally na Abbas Sykes kati ya Mtaa wa Sikukuu na Livingstone.
Kaka yake Mnubi akiitwa Kapesa alikuwa dereva wa mabasi ya DMT yanayosafari kwenda bara.
Wakati niko Moshi mdogo siku za likizo nilikuwa nikipandishwa basi analoendesha Kapesa nakabidhiwa kwake kuja Dares Salaam. Mama yangu alikuwa akinitengenezea maini ananifungia na mkate wa boflo chakula changu cha safari mkate ukiwa fresh kabisa.
Mama yangu Bi. Mwanaidi bint Mohamed Allah amrehemu alikuwa nesi na alikuwa makini sana na kanuni za afya hakuamini nile chakula cha njiani.
Nilikuwa nashuka Kariakoo sokoni ambako kulikuwa na kituo DMT ikishusha abiria.
Pale nilkikuwa natembea kw amiguu tu hadi Mtaa wa Gogo kwa mama yangu mdogo Bi. Mtoro bint Mohamed.
Mnubi aliendelea a masomo Azania Secondary School mwaka 1966 lakini alisoma kwa kiasi cha miaka miwili tu zaidi au pungufu akaacha shule.
Mnubi alikuwa akicheza Yanga na alikuwa mlinzi wa kutumainiwa. Kwa ajili hii Yanga ikamshughulisha sana.
Mnubi Half Back wa kutegemewa akaacha shule Yanga wakamtafutia kazi Cargo akaajiriwa na East African Cargo Handling Services.
Inasemekana Yanga ndiyo waliomshawishi aache kusoma kwani akiwa mwanafunzi haikuwa rahisi kumpata kila atakapohitajika kucheza mechi hasa Yanga inaposafiri.
Wenzake wengi katika timu ya Yanga tayari walikuwa waajiriwa wa EACHS akina Kilambo, Msomali, Jamil "Denis Law" Hizam, Abdulrahman Juma, Hassan Goboss kuwataja wachache.
Mwalimu Reveta alikuwa heshi kutueleza habari za Mnubi darasani na umahiri wake katika somo la hisabati na kwa masikitiko makubwa akituambia kuwa aliumia sana kusikia kuwa Mnubi kaacha shule kidato cha pili ili acheze mpira Young Africans.
Miaka mingi baadae nikakutana na Mnubi bandarini mwaka wa 1972 sote sasa tukiwa vijana wadogo.''
Picha nyingine Jamil ''Denis Law'' Hizam aliyekaa katikati na simu, Athumani Kilambo kushoto na Abuu (Cosmopolitan) wote kutoka Bagamoyo sasa katika utu uzima.