..hii ni introduction ya makala ya Ahmed Rajab ktk gazeti la Raia Mwema.
..It is an interesting reading, mnaweza kuifuatilia ktk link niliyotoa hapo chini.
TANBIHI YA MKUTANO WANGU NA HANGA-- Ahmed Rajab
KUMBUKUMBU na usahaulifu. Kalima hizo mbili zina umuhimu mkubwa katika fani ya uandishi wa historia. Katika fani hiyo, "kumbukumbu" na "usahaulifu" huwa na siasa zake na nguvu za aina yake. Uandishi wa historia una miiko na maadili yake. Ni mwiko kwa wanahistoria pamoja na waandishi wa mambo ya kihistoria kupotosha historia kwa kutoa maelezo kinyume na matukio halisi yalivyotukia. Na huo ni mwiko mkubwa. Miongoni mwa maadili ya uandishi wa historia ni kwanza, kuyafatiisha mambo na kuyachunguza kwa kina; na pili, kutoa maelezo yaliyo sahihi bila ya upendeleo. Hii si kazi nyepesi hasa kwa wale wenye misimamo ya kisiasa. Kwa hakika, hiyo si kazi nyepesi hata kwa wasio na misimamo ya kisiasa kwa sababu mara nyingine kutokuwa na msimamo wa kisiasa kwenyewe ni sawa na kuwa na msimamo wa kisiasa. Uandishi wa historia unazidi kutatanisha pale mwandishi anayeandika kuhusu matukio ya kihistoria anapowategemea wasimulizi wenye hakika kwamba ni wao tu wenye ukweli. Wasimulizi hao hutegemea kumbukumbu zao bila ya kusaidiwa na ushahidi wa maandishi wenye kuthibitisha wanayoyakumbuka.
SOURCE :http://raiamwema.co.tz/tanbihi-ya-mkutano-wangu-na-hanga#sthash.W4a4N8tY.dpuf
cc Mohamed Said, Ritz, Nguruvi3, Mag3, Barubaru, Mzee Mwanakijiji

Last edited by a moderator: