Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nguruvi3, Mohamed Said,
..historia ya Znz ni vizuri ikaandikwa na outsiders ambao hawataelemea upande mmoja
..kinyume cha hapo tutabaki na historia za Ramadhani Mapuri vs Dr.Harith Ghassany.
Joka Kuu,
Huwezi kufananisha kitabu cha Dr. Harith Ghassany na kitabu cha Ramadhani
Mapuri.
Hata siku moja.
Msome Mapuri kisha msome Dr. Ghassany uone tofauti iliyopo - chalk and cheese.
Hao "outsiders" weshaandika.
Hakuna jipya litakalotoka kwao baada ya nusu karne.
Prof. Mohamed Bakari anasema ni bora tukaandika historia zetu wenyewe badala
ya kusubiri Wazungu watuandikie kwa kuwa wataandika mambo sisi hatukubaliani nayo.
Mudeer, Mohamed Said.Joka Kuu,
Huwezi kufananisha kitabu cha Dr. Harith Ghassany na kitabu cha Ramadhani
Mapuri.
Hata siku moja.
Mmoja ni kada wa CCM na mwingine ni msomi wa Harvard.
Binafsi nina uzoefu mkubwa wa kazi za makada.
Kuna kitabu cha Historia ya TANU 1954 - 1977 kilichoandikwa na Kivukoni Ideological
College.
Ukiwa hujakisoma kitafute usuuzike na nafsii yako.
Kuna kitabu cha maisha ya Rashid Mfaume Kawawa alichoandika Dr. John Magoti
Kitafute ustarehe.
Mimi sitaki kutia neno nakuachia wewe na Majlis mvisome vitabu hivyo kisha mleta
khabari hapa jamvini.
Sasa kumleta Mapuri...
Huu ni mzaha mbaya.
Msome Mapuri kisha msome Dr. Ghassany uone tofauti iliyopo - chalk and cheese.
Hao "outsiders" weshaandika.
Hakuna jipya litakalotoka kwao leo baada ya nusu karne.
Prof. Mohamed Bakari anasema ni bora tukaandika historia zetu wenyewe badala
ya kusubiri Wazungu watuandikie kwa kuwa wataandika mambo sisi hatukubaliani nayo.
Katika kufunika hilo la rangi, Mohamed anasema huyu ni msomi wa Havard..u can not see these things wakati Dr.Ghassany ni rafiki yako.
..hawa ndugu zetu bado wamegawanyika kati ya wanaoumuunga mkono Sultani na wanaounga mkono mapinduzi.
Katika kufunika hilo la rangi, Mohamed anasema huyu ni msomi wa Havard
Ritz,Mudeer, Mohamed Said.
Nipo pembeni nakusoma na nakufuatilia kwa ukaribu mno unavyotoa darsa.
JokaKuu,..u can not see these things wakati Dr.Ghassany ni rafiki yako.
..hawa ndugu zetu bado wamegawanyika kati ya wanaoumuunga mkono Sultani na wanaounga mkono mapinduzi.
Mohamed, sasa kama huna uhakika na habari unazoandika, unapata wapi nguvu za kusimamia hoja hiyo tena ukisema historia ya kweli
Ni mara ngapi katika mnkasha huu umetuwekea mabandiko ukiwanukuu watu waliohusika?
Leo unawezaje kutuambia hujui, ikiwa wewe ndiye unaeleza kuhusu Kipumbwi?
Ndio maana tunasema, kuna walakini, tena mkubwa. Leo Mohamed hawezi kusema mapinduzi ni halali au ni haramu. Kesho anatualmbia Nyerere mbaya sana, kaenda kuua watu Znz!
Mohamed, wapi unaposimama katika hili. Mapinduzi ni halali au ni haramu
Unawaeleza nini Wazanzibar, kwamba waendelee kuyaenzi au waachane na 'udhalimu' wa Nyerere?
Vijana wamechanganyikiwa, tuwekee sawa mzee wetu
https://www.youtube.com/watch?v=Dtqh8fva8RoNguruvi3,
Ala!
Kumbe wewe unaona rangi!
Rangi gani uionayo?
Nguruvi 3,
Unataka mimi ndiye niseme kuwa mapinduzi ni haramu.
Haya nikishasema hilo ndiyo iwe nini?
Nani kakuambia kuwa mimi sina uhakika na niyasemayo?
Mimi nakupa habari ambazo hujapata kuzisikia popote duniani.
Nyie mlimjua Mzee Mkwawa Kamanda wa Jeshi la Kipumbwi?
Ali Mwinyi Tambwe, Jumanne Abdallah, Victor Mkello...watafiti
wameandika historia ya Mapinduzi ya Zanzibar lakini wahusika hawa
hawakuwako katika kurasa zao.
Ngoja nikuongeze kitu kingine usichojua.
Kuhusu mauaji...
Wazee wetu wengi walihusika katika namna moja au nyingine katika
yale mapinduzi lakini hii leo hakuna anaetaka jina lake lihusishwe na
mapinduzi kwa sababu ya yale mauaji yasiyokuwa ya lazima kamwe
yaliyotokea wakati serikali tayari ilikuwa imeshaanguka.
Unajua Abdul Sykes alimwambia nini Issa Nasser Al Ismaily
alipomuuliza kuhusu yaliyotokea Zanzibar?
Issa Nasser ndiye aliyeandika, "Kinyang'anyiro na Utumwa Zanzibar."
Ikiwa huyajui majibu ya Abdul Sykes nifahamishe nitakueleza.
Ali Mwinyi Tambwe kapewa medali ya mapinduzi katika kusheherekea
miaka 50 ya mapinduzi lakini alipokuwa hai hakutaka kabisa jina lake
lihusishwe na kadhia hiyo.
Sisi ni Waislam na tunajua dhima ya kutoa roho pasi na haki.
Kyenju,Mohamed Said huwa anaandika historia zisizokuwa balanced, historia zake huwa zinaongozwa na mihemko, iwe ya kidini au kundi analoliunga mkono atalipamba na kufunija uchafu wake. Inashangaza, eti mtu anaandika historia ya Wazee wake huku hakiacha kuitaja jamii ya watu wengine ambao walikuwa pamoja na wazee wake, au anawataja bila kueleza mazuri waliyoyafanya.
mzee wangu mapinduzi yalikuwa halal au haram!!?? nisaidie kijana wako naona wajibu usivyoulizwa..
ahsanta
Joka Kuu,
Huwezi kufananisha kitabu cha Dr. Harith Ghassany na kitabu cha Ramadhani
Mapuri.
Hata siku moja.
Mmoja ni kada wa CCM na mwingine ni msomi wa Harvard.
Binafsi nina uzoefu mkubwa wa kazi za makada.
Kuna kitabu cha Historia ya TANU 1954 - 1977 kilichoandikwa na Kivukoni Ideological
College.
Ukiwa hujakisoma kitafute usuuzike na nafsii yako.
Kuna kitabu cha maisha ya Rashid Mfaume Kawawa alichoandika Dr. John Magoti
http://www.mohammedsaid.com/2013/12/mapitio-ya-kitabu-simba-wa-vita-katika.html
Kitafute ustarehe.
Mimi sitaki kutia neno nakuachia wewe na Majlis mvisome vitabu hivyo kisha mlete