Ahsante Rais Samia, hatimaye HESLB wafuta VRF kwenye system yao

Aliyepeleka wazo la VRF Kama bado yupo kazini ni kosa kubwa Sana uyo jamaa anatakiwa afukuzwe kazi Mara moja sio mzalendo
 
Swala la kulinda thamani ya pesa lilitakiwa kuachwa na cha msingi ingepunguzwa asilimia........ yani ukope leo laki halafu baada ya miaka kumi ulipe laki hiyo hiyo? Aiseee
Nasikitika Sana kuona Kuna watu Kama wewe kwenye Taifa langu . stupid
 
Usipompata msikivu inakuwaje?
Tutafute suluhisho la kudumu
 
Hatimaye nimefanikiwa kuona taarifa zangu bodi.

Siamini kile ninachokiona, je ndicho hicho hicho au system ya bodi itabadilika na kuwa kama zamani? Ila kama ndivyo kilivyo basi mama President hongera yake kwenye hili la bodi, mana deni langu limepungua milion 4. Ile VRF na penati vilikuwa ni hatari sana.

Huu ndiye rais msikivu. Huko Morogoro napo kaahidi maji nchi nzima. Haya ndo maendeleo ya watu.

Mama akienda vizuri atapata kura tu. Asiogipe kuleta katiba mpya, kwa sababu ni lazima atashinda tu. Ni msikivu mnoo na anazingatia logic mnooo.
 
Hij total charge amount wametumia formula gani kuipata mbona zinatofautiana Sana ?
 
Unamshukuru Samia badala ya kushukuru mifumo na taasisi zinazohusika?WTF!!!Tatizo la Watanzania wengi kuwa na akili fupi namna hii ni nini?Ni elimu hamna?Ni elimu duni?Ni syllabus zetu?
Hee..hili jamaa vipi? Kwani bodi wamefuata amri ya nani? C ya rais aliesema waifute..hiyo mifumo haikuwepo kabla ya samia au? Nazani wewe ndo mwenye shida kwenye bichwa lako hilo
 
Hee..hili jamaa vipi? Kwani bodi wamefuata amri ya nani? C ya rais aliesema waifute..hiyo mifumo haikuwepo kabla ya samia au? Nazani wewe ndo mwenye shida kwenye bichwa lako hilo
Kwa nini ushukuru kwa kupewa haki yako?Kwanza unaelewa kuwa haki huwa haiombwi wala kutolewa bure bali huchukuliwa?Kwa nini umshukuru Rais kwa kutimiza wajibu wake?Yaani umwajiri Rais ambae unamlipa mshahara kwa kukufanyia kazi kadhaa wa kadha kisha akishafanya hizo kazi unamshukuru wakati tayari ni wajibu wake!Akili za wapi hizi!!!
 

Mkuu kila nikiingiza FORM FOUR index namba yangu inaniletea “ Incorrect Index Number Format”….Nikienda kwenye advanced search by names kwenye vyuo/taasisi vilivyopo ni vya Tanzania tu hakuna vyuo vya nje.

Advise please? Au system ina cut-off ya miaka kwa waliomaliza zamani kidogo haitambui? Mimi nimemaliza form four mwaka 2002.
 
Hij total charge amount wametumia formula gani kuipata mbona zinatofautiana Sana ?
Hata mimi niliuliza hilo swali hakuna aliejibu hata Bodi (HESLB) yenyewe nimewapelekea malalamiko jawajanijibu. Ukiangalia vizuri utagundua hapo kwenye hiyo Total charges amount hazifanani mfn mimi nina deni dogo ukilinganisha na wenzangu ila hiyo Total charges amount ni kubwa ukilinganisha na hao wenzangu.
 
Hivi ukiingiza namba ya form four unafanyaje kwenda hatua inayofuata?
 
Ile Total charges ina vitu viwili
1. Administration fees 10%
2. VRF repaid before 1st May.
Mfano mimi na wewe tumekopa milioni 10.
Mimi nikaanza kukatwa January 2021.
Nitalipa VRF miezi minne (Jan,Feb,mar,April)
Wewe ukaanza kukatwa April, utalipa VRF mwezi mmoja tu.
Hapo lazima total charges zitofautiane. Kadri tulivyoanza kukatwa mapema ndivyo deni la total charges linakuwa kubwa.
 
Nenda pale forgot index then fuata maelekezo watakutengenezea nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…