Ahsante Rais Samia, kwa hili Watumishi wa Umma tumekuelewa sana

Sawa bana, nikukumbushe tu ndugu yangu unayesubiria NMB.

week hii mambo hayakua sawa nimeingiza 1980000 tu.
Mambo yamebana kidogo
 
Mna shida sana .... Subiri uone ...... Kaa kwa utulivu. Ndio uje uhadithie .... Shida yenu mnaingiza siasa kwenye utaalamu. Mshahara utabadilika lakini mtangoja sana . Ukibadilika tarehe ya kwenye barua njoo hapa.. Kama ndio unasubiri kupanda Mara ya kwanza wenzako tushapanda mara3. Karibu
 
Karibu... Kwa hiyo mshahara wa juni utabadirika!! Kisa payroll zinafanyiwa kazi before 15th ya mwezi!!?? Ngoja muone ... Nawaambia kwa uzoefu ... Na mpaka sasa ni walimu tena baadhi waliopewa barua za madaraja... Yaaani mkiwahi ni mwezi wa 11-12 huko.
 
Yaa huwa inachelewa ndo maana watu huwa wanadai arreas....
 
Nilitakiwa kupanda mara 2 ila baba ako alininyima kupanda mara mbili.

Hili nitaenda kusema hadi kwa Mungu, nione kama atampa hao malaika awaongoze.

#YNWA
 
Mkuu umeongea vema sana tena hisia kali. Ila nitajibu kistaarabu kabisa.

Hao wananchi si ndiyo wale wale wanaoshangilia kuona mtumishi anatumbuliwa?

Hao wananchi si ndiyo wale wanaowachukia watumishi na wakuwaita wezi? Hivi mwalimu wa chekechea anaiba nini, chaki?

Hao wananchi si ndiyo walioshangilia kipindi cha mwendazake kuwa watumishi wa umma nidhamu imerudi kazini lakini wakasahau kuwa watumishi wanaishi kama vinyamkera kwenye nchi yao wenyewe?

Umeongelea mwalimu ambaye ameshakuwa punching bag ya wanasiasa. Vibao, viboko, kufungwa, kudhulumiwa, kudekishwa madarasa, kuonewa nk hufanyiwa yeye na bado unataka akufundishie mwanao kwa weledi?

Wanafunzi wakifaulu lawama kwa mwalimu. Wakifeli lawama kwa mwalimu. Wasijue kusoma lawama kwa mwalimu.

Mwalimu yuleyule ambaye hajawahi kujengewa makazi na serikali, hajapanda daraja miaka 7, hana posho, hana nyongeza ya mshahara kwa miaka 7, analipa kodi na bili zote kwa mshahara wa laki 2.

Huyo uliyemtaja ni mungu na sio Mungu. Kipindi hiki watumishi wanafanya kazi kulingana na wanavyolipwa. Huwezi kufanya kazi kiweledi kwenye nchi yenye double standard kama hii ambayo wanasiasa kutwa kucha wanakuka mema ya nchi hata wakitegemea watumishi wa chini wakalipwe mbinguni, mbingu ipi inayoonea watu wake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa bana, nikukumbushe tu ndugu yangu unayesubiria NMB.

week hii mambo hayakua sawa nimeingiza 1980000 tu.
Mambo yamebana kidogo
Wewe ni **** unanijua?

POLE.

NENDA IRINGA KILOLO ULIZA LIVERPOOL WA MAPARACHICHI FALA WEWE.

Unajua msimu huu nimechuma michumo mingapi, ya Tani ngapi, na mkenya kaniingizia TShs ngapi CRDB?

Unajua kuwa muda huu Nauza rejected Tani ngapi, na TShs ngapi?

Unataka nifunguke...

Njoo huku nikuonyeshe misitu ya pine na mlingoti yenye miaka zaidi ya mi5.

Nyauu kabisaaa

Kuna watu hatupendi na hatutaki BUSINESS tunapenda INVESTMENT.

INVESTING IS BETTER THAN BUSINESS.

ACHA DHARAU.

#YNWA
 
Potelea mbali itajulikanaga mbele kwa mbele.
 
Nenda taratibu Mkuu,mambo mazuri hayataki haraka.
 
Yaani kuongezewa TZS 30,000/= unashangilia kama zuzu mkuu? Kupandishwa daraja haina maana kabisa.
 
Yaani kuongezewa TZS 30,000/= unashangilia kama zuzu mkuu? Kupandishwa daraja haina maana kabisa.
Weka K mwisho sema 300k au 400k

Zuzu ni MATAGA wanaoshangilia kila kitu ili wapate kitu.

#YNWA
 
Angetamka nn mama wa watu ingali alikuwa anashuhudia wenzake wakishushwa wazimawazima wakileta kihelehele
 
Weka K mwisho sema 300k au 400k

Zuzu ni MATAGA wanaoshangilia kila kitu ili wapate kitu.

#YNWA
Acha uongo yaani daraja upandishwe 300K serikalini? Hata private ni watumishi wachache sana wanaopandishwa kwa kiasi hicho.
 
Acha uongo yaani daraja upandishwe 300K serikalini? Hata private ni watumishi wachache sana wanaopandishwa kwa kiasi hicho.
TGS C = 535,000
TGS D = 745,000
TGS E = 975,000
TGS F = 1,215,000

Anza A na endelea G ......

#YNWA
 
Acha uongo yaani daraja upandishwe 300K serikalini? Hata private ni watumishi wachache sana wanaopandishwa kwa kiasi hicho.
Kwani wewe unajua nini maana ya Daraja la Mshahara??

Wakisema Daraja unajua ni nini? Mtu anabadilikaje daraja?

Sent from my SM-J200F using JamiiForums mobile app
 
Unajua watumishi ni walipa kodi waaminifu? Kila mwezi wanakatwa kodi unapo sema wanatafuna kodi zenu.. Ukimaanisha wenyewe sio wachangiaji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…