Sol de Mayo
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 6,515
- 6,230
Kuhusu Historia iliyowahi kutokea hapo zamani iitwayo Ottoman empire/Osman, nilikuja na ombi la kuongezewa muda sisi kama wadau na wafuatiliaji wa tamthilia hii inayopendwa, inayosisimua na kufuatiliwa na watu wengi.
Sina budi kuwashukuru Azam tv, kwa kulifanyia kazi ombi langu, si mimi tu, huenda na wengine pia walitamani iwe hivyo, na hakika imekuwa! Japo ni kidogo, lakini si haba, nawashukuruni sana, na matumaini yangu mutatuongezea wadau wenu angalau lisaa li-moja na 30 minutes.
Ahsanteni, huku kanda ya ziwa/usukumani kabila lenye population kubwa, tunasema hivi, Waabeja sana Azam, brand kubwa, hakuna kama azam.
Nawapendeni wote.