Ahsante sana Tundu Lissu, John Heche na wengineo. Jipeni moyo, msikate tamaa

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
667
Reaction score
1,403
Nashukuru sana waheshimiwa Tundu Lissu, John Heche na wapigania uhuru wengine wa CHADEMA.

Jipeni moyo, msikate tamaa. Inawezekana siku ile unayokata tamaa ndo siku ya kukamilika kwa ukombozi kamili wa Nchi hii.

Kutokana na ugumu wa safari na nature ya watu wengine kuwa na interest tofauti tofauti, bila shaka katika kipindi hiki wanaweza kutokea wanachama wengi sana wanaohama kwa visingizio mbalimbali, hata kama ni vya uongo. Inawezekana wakakimbia hata wale ambao hukuwahi kuamini kwamba wangefanya hivyo. Msife moyo, Mungu ana wakati na maksudi yake katika kila jambo linalotokea.

Mungu anaweza kuleta UKOMBOZI kwa kutumia hata watu 10 tu ndani ya chama, wenye nia moja, mtazamo mmoja, msimamo mmoja, uelewa mmoja na waliojitoa kweli kweli bila kujibakiza.

Mungu anaweza kughaili kuangamiza mji mzima kutokana na mwenye haki mmoja tu aliyepo.

Vivo hivyo Mungu anaweza kuleta UKOMBOZI katika Nchi nzima kupitia wenye wachache tu wenye moyo mmoja wa ukombozi.

Kwa hiyo, hata kama wakakimbia wangapi, msiogope, simameni imara, watakieni safari njema, wala msiwaseme au kuwatukana. Wapeni mkono wa heri kwa moyo mweupe kabisa lakini ninyi songeni mbele.

Ahsante.
 
Amina, Wengine wameenda kula Ubwabwa.
IMG-20250520-WA0057.jpg
 
Back
Top Bottom