Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
JAN24
Nilikujia na post moja ya kuomba ushauri kwenye kesi za mirathi ya vijana fulani mtaani.
Kuna vijana fulani walifiwa na wazazi, sasa baba yao mdogo akawa msimamizi. Katika hilo, akagoma kuweka kiwanja cha marehemu kwenye documents za mirathi.
Mungu ni mwema, ni muda mrefu, hatimaye msimamizi wamemwondoa na watoto wote wamekuwa wasimamizi. Na kila mali ya marehemu imeamriwa wagawane pasu pasu.
Haikuwa rahisi. Wale watoto machozi yaliwatoka wakiwa mahakamani, wakaanza kutukumbatia, wengine wakipiga magoti kusali mahakamani.
Nichukue fursa hii kushukuru uongozi wa JF na wale wanasheria wote walioshiriki kutushauri. Tujitahidi sana kusoma majukwaa ya "Health" na "Sheria" ni msaada mkubwa sana... kwetu.
Ni kazi ya kujitolea lakini Mungu ndiye anayeamua. Nashauri wote mnaosimamia mali za marehemu msiwe na tamaa, Mungu anajibu duniani. Mali za watoto ziheshimiwe haijalishi wana umri gani.
Soma Pia: Mfumo wa Mjue Mwenye Ndoa Kidijitali utasaidia kupunguza Migogoro ya Ndoa na Kesi za Mirathi
Yule mzee mara tatu alisimama, akapata kama mshtuko, kisukari kikapanda, wakaahirisha kesi.
Tukikaribia kufunga kesi, alilia sana, anaomba akae na watoto wote wayamalize nje ya mahakama. Bahati mbaya haikuwa rahisi kwake.
Ninajua pengine na wewe ni mmoja wa waathirika wa eneo hili. Never give up.
Hawa wasimamizi tulichokiona ni jeuri ya pesa. Wanamini pesa inaongea kila eneo, wakasahau inaweza badili matokeo pia.
GDNYT

- Akatofoa cheti cha kifo cha marehemu kaka yake aliyefia Moshi badala ya Dar es Salaam na kuzikwa Moshi.
- Wale watoto ni wa ndoa, lakini wana ndugu zao nje ya ndoa. Msimamizi akawaandikia moja ya kiwanja kikubwa watoto wa nje ya ndoa akidai walipewa na baba yao.