Ahsanten sana manguli wa sheria humu mmetusaidia sana kwenye ushindi kesi za mirathi ya vijana fulani mtaani

Ahsanten sana manguli wa sheria humu mmetusaidia sana kwenye ushindi kesi za mirathi ya vijana fulani mtaani

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
JAN24
Nilikujia na post moja ya kuomba ushauri kwenye kesi za mirathi ya vijana fulani mtaani.

Kuna vijana fulani walifiwa na wazazi, sasa baba yao mdogo akawa msimamizi. Katika hilo, akagoma kuweka kiwanja cha marehemu kwenye documents za mirathi.

  1. Akatofoa cheti cha kifo cha marehemu kaka yake aliyefia Moshi badala ya Dar es Salaam na kuzikwa Moshi.
  2. Wale watoto ni wa ndoa, lakini wana ndugu zao nje ya ndoa. Msimamizi akawaandikia moja ya kiwanja kikubwa watoto wa nje ya ndoa akidai walipewa na baba yao.
Tulitafuta wanasheria kuwasaidia, na wengine walikuja kutoa ushauri na wengine walitoa na namba za simu kuwasiliana jinsi gani ya kuwasaidia.

Mungu ni mwema, ni muda mrefu, hatimaye msimamizi wamemwondoa na watoto wote wamekuwa wasimamizi. Na kila mali ya marehemu imeamriwa wagawane pasu pasu.

Haikuwa rahisi. Wale watoto machozi yaliwatoka wakiwa mahakamani, wakaanza kutukumbatia, wengine wakipiga magoti kusali mahakamani.

Nichukue fursa hii kushukuru uongozi wa JF na wale wanasheria wote walioshiriki kutushauri. Tujitahidi sana kusoma majukwaa ya "Health" na "Sheria" ni msaada mkubwa sana... kwetu.

Ni kazi ya kujitolea lakini Mungu ndiye anayeamua. Nashauri wote mnaosimamia mali za marehemu msiwe na tamaa, Mungu anajibu duniani. Mali za watoto ziheshimiwe haijalishi wana umri gani.

Soma Pia: Mfumo wa Mjue Mwenye Ndoa Kidijitali utasaidia kupunguza Migogoro ya Ndoa na Kesi za Mirathi

Yule mzee mara tatu alisimama, akapata kama mshtuko, kisukari kikapanda, wakaahirisha kesi.

Tukikaribia kufunga kesi, alilia sana, anaomba akae na watoto wote wayamalize nje ya mahakama. Bahati mbaya haikuwa rahisi kwake.

Ninajua pengine na wewe ni mmoja wa waathirika wa eneo hili. Never give up.

Hawa wasimamizi tulichokiona ni jeuri ya pesa. Wanamini pesa inaongea kila eneo, wakasahau inaweza badili matokeo pia.

GDNYT
 
Umefanya la maana kumshukuru,kuna watu humu niliishukuru JF kwa kuanzishwa eti kila mara mnawashukuru!Shukuruni bila kukoma kila iitwapo Leo!
 
nilivyoviona mahakaman inasikitisha sana sana yaan kuna watu wanateseka sana kisa hawa mbwa wanaitwa

[wasimamizi]

yupo mama mmoja ana watoto 3 mume kamuachia 2017

msimamizi ajafungua kesi mke kaenda kulalama anachoongea utasikitika hikiiporo tumeamua kukibeba octb tuko nao huko moshi naamini huyo mbwa atatag
futa njia ya kuja tyu

yaan wana nyumba 3 mwanzoni kakamtu [msimamizi]alisema atakuwa anakusanya kodi a awape wakasikilixia mke akiwa na shida akipigiwa anajibu konyo

Chakwanza tuliiwapatia mwanasheria wakuwasaidia kwa kuanzia...so far wametoa order wapangaji wote wasilipe kodi kwa huyo kaka wa marehemu apewe mkewe na watoto wao

Yaan vitoto vidogo ukiwangalia chozi linakutoka

na walikuwa shule nzuri.sahizi wanadunda upili

 last

wakampata ndugu mmoja akaenda kusimamia show mahakaman inachonekana msimamizi alishaenda mahakaman so kila mke wa marehem akikanyaga anaambaiwa na hakimu leta msimamiz...aisee

Dis tym tulisambaza kwa wakubwa zake naona ametoa wito wa kuitwa huyo bwana mahakaman

Usichexe na haki za watu zinachelewa tu
 
Umefanya la maana kumshukuru,kuna watu humu niliishukuru JF kwa kuanzishwa eti kila mara mnawashukuru!Shukuruni bila kukoma kila iitwapo Leo!
Amen kaka
Hata baibooo inasema Mungu anapenda shukran..
 
nilivyoviona mahakaman inasikitisha sana sana yaan kuna watu wanateseka sana kisa hawa mbwa wanaitwa

[wasimamizi]

yupo mama mmoja ana watoto 3 mume kamuachia 2017

msimamizi ajafungua kesi mke kaenda kulalama anachoongea utasikitika hikiiporo tumeamua kukibeba octb tuko nao huko moshi naamini huyo mbwa atatag
futa njia ya kuja tyu

yaan wana nyumba 3 mwanzoni kakamtu [msimamizi]alisema atakuwa anakusanya kodi a awape wakasikilixia mke akiwa na shida akipigiwa anajibu konyo

Chakwanza tuliiwapatia mwanasheria wakuwasaidia kwa kuanzia...so far wametoa order wapangaji wote wasilipe kodi kwa huyo kaka wa marehemu apewe mkewe na watoto wao

Yaan vitoto vidogo ukiwangalia chozi linakutoka

na walikuwa shule nzuri.sahizi wanadunda upili

 last

wakampata ndugu mmoja akaenda kusimamia show mahakaman inachonekana msimamizi alishaenda mahakaman so kila mke wa marehem akikanyaga anaambaiwa na hakimu leta msimamiz...aisee

Dis tym tulisambaza kwa wakubwa zake naona ametoa wito wa kuitwa huyo bwana mahakaman

Usichexe na haki za watu zinachelewa tu
Mkuu una ujumbe wa maana, sema unauharibu ujumbe wako wote kutokana na aina ya uwasilishaji wako hapa jukwaani!!
 
Back
Top Bottom