Uchaguzi 2020 Ahsanteni Watanzania kwa kutuchagua ila tusisahau CCM bila Upinzani ni sawa na Dini bila Shetani, hakuna visingizio!

Msema Kweli Ni Mpenzi Wa Mungu
Baadaye Utarudi Hapa Kufanya Masahihisho
Enzi za Nyerere alikuwepo mbunge Masoud pale Temeke moto wake sijawahi kuuona hadi leo hakuna cha Lissu, Dr Slaa wala Zitto hawamfikii.

Pale Tandahimba alikuwepo Stephen Nandonde ukirudi Dodoma unamkuta Kuwayawaya S Kuwayawaya serikali ilikuwa inasimama dede hadi mawaziri wanatoa lugha chafu bungeni!
 
Naunga mkono hoja. Watoto wa maskini wanakaa chini shuleni huko kwa kukosa madawati, wanabanana wanafunzi hadi 100 kwa ukosefu wa madarasa halafu Kodi za wazazi wao zinatumika kipuuzi namna hii!!?

Bora tufute uchaguzi pesa zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo

"Hakuna dini bila shetani"
 
Kabisa ,nimehuzunika sana kupoteza bando nafuatilia uchaguzi ambao hauna hata fair condition.Mimi nasema wazi tulipoteza muda bure kuwasikiliza wagombea.
 
Tutateua wabunge wa upinzani ili waunde kambi ya upinzani bungeni. Tutamteua Zito, Mbowe, Esther Matiko, Msigwa na Lisu.
 
Wapinzani kukosa wabunge wengi bungeni ndio kusema nchi haina wapinzani? Mch Mtikila (RIP) hakuwahi kuwa mbunge ila alikuwa mpinzani makini na shupavu.
 
Mzee Mbaya umenena..haiwezekani kutoa hela zetu wenyewe CCM kwà ajili ya uchaguzi kisha ashinde mpinzani hata mmoja..ila jamani tumetenda dhambi Sana Basi tuu..😀😀😀. CCM mpya ni nyooko aisee
 
Demokrasia ndio basi tena tunabaki na Kibajaji na musukuma
Magufuli anakotupeleka anajua mwenyewe
 
Warudi bungeni ili muwasingizie kuwa wamechelewesha Maendeleo?
 
Ahahahh
 
Kilikuwa.chama kimoja tu,ukitaka iwe hivyo sharti ufute Kwanza vyama vingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…