MUWHWELA
Senior Member
- Oct 26, 2013
- 167
- 238
TWIME TUBITE
Napenda kuufahamisha umaa na mhariri mkuu kwamba mjadala huu ulifaa uwe kwenye technology,Lakini mantiki yake inafaa kujadiliwa na kusomwa na watu wenye maulizo yasiyo ya kawaida.
-------------
Akili bandia, Kuna binadamu wenzetu wanawaza na kutenda kwa namna ya kipekee sana, ama kwa kuwa wanapenda vitu rahisi au wanataka kutafuta maana ya maisha ya mwanadamu hapa duniani. Yote mawili yanafikirisha.
Akili bandia Mimi naipa jina kama "silaha ya mwisho ya maangamizi kwa mwanadamu" hatuna muda mrefu sana ulimwengu huu utaingia kwenye shida kubwa ambayo itakuja kuichukua Dunia miaka 100 kuziba demage iliyotokea within 10-20yrs ya matumizi ya hii akili bandia.
Wataalam wa sayansi hii ya TEKINOLOJIA wanasema, mashine zinazozalishwa Sasa zinaenda kuwa na akili kubwa maradufu ya mwanadamu mwenye UHAI, hayo yapo na yanaendelea kuwepo Katika sekta nyingi za kiuchumi.
JIULIZE KAMA MIMI
Wamiliki wa TEKINOLOJIA hizi ni wafanyabiashara wakubwa duniani ambao hawana mfumo rafiki na MTU, serikali, au kikundi Cha watu, wao rafiki Yao ni faida, mahala penye faida UHAI wako Hauna thamani kwao. Je serikali za Afrika zimejiandaa kupeleka watu wao kwenye mfumo huu mpya wa lazima?
Akili bandia- mashine kama robot ikiwa na akili kubwa / uwezo mkubwa wa kufikiri na kutenda, Hawa wanadamu watafanya kazi Gani Ili kuendesha maisha yao? Maana msingi wa maisha yetu ni matumizi sahihi ya muda na nguvu Ili kujipatia mahitaji muhimu kwa wakati huo ambao UHAI upo upande wako. (Hili ni tatizo la kwanza)
Akili bandia - Katika ulinzi hapa ndipo unaweza kuona kwamba kwasababu hatuaminiani tutauana kama wadudu, maana kutakuwa na mashine ambayo inajua unachowaza, wapi ulipo, unafanya nini kwa lengo Gani ,pia mashine hizo zitatumwa popote bila MTU halisi kuwepo, are we good enough?? Ku-challange hii kitu, vikosi vyetu vya usalama vina developer's wetu, ambao siku za usoni wao ndiyo watakuwa bunduki wakiwa nyuma ya computer na keyboard zao.(Hili ni tatizo la pili)
Akili bandia-Katika kamari na michezo, kwa miaka ya hivi karibuni kamari na wamiliki wa mifumo ya kamari ndiyo watu wenye fedha nyingi kuliko mkulima. Takwimu zinasema nguvu nyingi ya akili bandia na wamiliki wao wameelekeza pia Katika kamari na michezo. Jamii kubwa imeachia kundi dogo la wazalishaji na kujiingiza Katika dimbwi la kusubili mashine zikosee Ili wao wapate utajiri..kizazi kimelemaa na kwa ulemavu huo ipo siku wahuni wataisimamisha Dunia na kutoa amri wanayotaka (Hili ni tatizo la Tatu)
Akili bandia- Elimu na utafiti, Leo Kuna chart GBT ambayo inafanya Kila kinachoitwa swali kwa ufanisi wa 60-90% hii ni hatari sana, mwalimu ana - anatumia mashine na mwanafunzi anatumia mashine..kamwe mashine haziwezi kuushinda UBONGO wa mwanadamu, Lakini kwakuwa tumeruhusu Elimu ya kizungu, tumeruhusu media ndiyo iamue aina ya Elimu tunayoitaka basi. Tukubaliane kwamba hakuna ugunduzi mpya utakuja kwa kizazi hiki, maana sote tunaamini mashine kuliko akili na Fikra za watu wetu...hatutaki kujiuliza kama robot inaenda kufanya kazi hiyo wewe ilipaswa ufanye..wewe unaenda kufanya nini?(Hili ni tatizo la nne)
Akili bandia- Usalama wa mataifa ya Afrika, Kuna kampuni kama tano hivi hizo ndizo maarufa kwa uzalishaji wa vihifadhi data (chip) makapuni hayo yote yapo Ulaya na Asia. Ili akili bandia ifanye kazi vema inahitaji vifaa hivyo kuwa imara na vyenye ufanisi mkubwa. JIULIZE huyo anayekuuzia saver Ulaya au Asia atakosa kujua taarifa zako? Usalama wako utakuwa wapi? Tupo prepared kushiriki hata kwenye mchakato wenyewe? (Hili ni tatizo la tano)
MWISHO- Binadamu anahitajika kuwa active ,atumike kwa faida ya wengine, ipo Radha ya maisha kama tunaruhusu akili zetu zitatue matatizo yetu kwa umoja na ushirikiano bila kuwa na haraka hivyooo. Maana end product ya mwanadamu in every second ni furaha.
Sipingi Wala sipo kinyume na technology,Lakini technology ambayo inataka kuondoa maana ya maisha na Radha yake, inapaswa kutazamwa upya na kuweka shinikizo Ili UTU wa MTU ubaki Katika HESHIMA yake ya awali.
Nafahamu, JUHUDI za kurahisisha maisha zinahitaji matakwa ya wengi na muunganiko wa mawazo wa jamii iliyokubwa, maana kiasi sote ni wamoja kwa mantiki ya sheria za Asili ambazo zinatuongoza sote kama viumbe hai tunao onekana na wale wasioonekana, hizo sheria ziko fear.
------+-++
IPE AKILI KAZI