AI (Artificial Intelligence) inaupeleka ulimwengu kwenye uharibifu mkuu, kwanini nawaza hivi?

Zilipo anza kuvumbuliwa mashine viwanda watu walikua na hii doubt lakini wakavuka

Zikaja kompyuta watu wakawa na hii shaka lakini tukavuka

Hata hili la AI tutaishi nalo na tutavuka

Hakuna kitu kinaweza kuzidi na ku replace intelligence ya binadamu
 
AI kuizidi akili ya binadamu ni aina fulani ya uongo ambao kiuhalisia hautatimia kamwe, to usidanganywe Wala kidanganya.
 
Tumekubali kuwa wavivu sana ,acha tu tukutane na yaliyopo..time will tell
 
Haya maneno Yako yanafaa kuwekwa kwenye mpangilio mzuri tu Ili jamiii kubwa ielewe..well Said
 
Kufanya Assassination itakua rahisi sana, dakika chache tu huna uhai tena, tena unauliwa na robot tena lako mwenyewe,

Ni kitendo cha haraka kama kutuma ujumbe wa sms.
 
Wakristo mlivyo na shida mnataka mpaka Ai iwatendee wema ndio muone ya kuwa inatenda haki,

Ai ni mwanzo sahihi wa kuitoa akili kwenye huu mwili uliojaa vikwazo vingi na kuiweka huru, halafu pia unaogopa vipi kitu ambacho hakina conscious? Hakioni, hakisikii, hakinusi, hakihisi,

Kwangu mimi tafsiri halisi ya Ai ni akili ya mwanadamu iliyohamishiwa kwenye mashine, kwahiyo kuiogopa Ai ni sawa na kuiangalia akili yako inavyofanya kazi nje ya mwili na kuamua kuiogopa...

Akili bandia ni mwanzo tuu katika hii safari ya kumuondoa organic being na kuleta super being ambaye hahitaji kutimiza mahitaji ya mwili kama tafsiri ya maisha.
 





View: https://youtu.be/sAbrXFK-l6U?t=197
 
Tumekubali kuwa wavivu sana ,acha tu tukutane na yaliyopo..time will tell
Huwezi ukalima kwa kutumia mikono au kijiti; ni lazima utumie jembe au nyezo nyingie ya juu kuliko jembe. Na ukilima kwa kutumia jembe au mikono badala ya kijiti unakuwa umetumia Teknoloji.

Hapa swali langu linakuja kwako,j Je kutumia teknoloji ni uzembe?
 
Ndugu yangu umeweke maneno siyo NENO...Katika mantiki ya kawaida kabisa TEKINOLOJIA kama ilivyo Haina shida,Bali maarifa na taarifa ulizonazo juu ya hiyo TEKINOLOJIA ndiyo mjadala ...."what you don't understand will not be controlled"

Watu wengi tunavijua vitu vingi Lakini hatuvielewi,
 
Akili bandia Mimi naipa jina kama "silaha ya mwisho ya maangamizi kwa mwanadamu"
Hii imekuwa kawaida kila mabadiliko mapya ya teknolojia yanapofika, hofu inakuwa kuu kuliko faida ya hiyo teknolojia.

Hizi hofu zetu zitupe nafasi ya kujifunza jinsi teknolojia zinavyofanya kazi.
Sasa hivi kuna modules mbalimbali za AI ziko public kama chatgp, na zinafanya task mbalimbali.
 
Tuseme kwa mfano; AI Gadget inayoweza kufanya kazi kwa replace ajira ya watu 100; uwekwe utaratibu kwa AI Gadget hiyo kuwalipa mshahara watu 100 wasiokuwa na kazi
Why hiyo Gadget itumike kama inaleta hasara. Unalipwa kufanya kazi tu. Teknolojia mpya ikija jitahidi ujifunze kujua inafanyaje kazi na kuitumia vizuri, hapo haitakuReplace.
 
Una hofu tu Mkuu, robot inakuwa programmed tu kufanya task fulani na kuweza kuRepond na mazingira ya hiyo kazi.

Roboti halina hisia kama mwanadamu liweze kukudhuru, unless limekuwa programmed kufanya hivyo.
 
Ujumbe huu umechambua vizuri sana changamoto na wasiwasi kuhusu maendeleo ya akili bandia (AI). Ni kweli, teknolojia hii inakuja kwa kasi na inaweza kubadili jinsi tunavyoishi, kufanya kazi, na hata kufikiri. Hata hivyo, kuna maswali makubwa ya kimaadili na kiusalama ambayo lazima yajadiliwe kwa umakini, hususan kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Tatizo la Ajira na Maisha ya Kawaida: Kama ulivyosema, akili bandia inaweza kuchukua nafasi za kazi nyingi, na kusababisha swali kubwa: binadamu watafanya kazi gani? Mashine zitakapoweza kufanya kazi nyingi za binadamu kwa ufanisi mkubwa, hatari ya ukosefu wa ajira itaongezeka. Lazima tuwe na mipango ya kujenga uwezo wa watu ili waweze kushirikiana na teknolojia badala ya kupoteza nafasi zao kwa mashine.

Usalama na Siasa: Katika upande wa ulinzi, AI inayo uwezo mkubwa wa kufanya uamuzi na kutoa matokeo yenye athari kubwa bila binadamu kuwepo moja kwa moja. Hii ni hatari, kwani mashine zinaweza kutumiwa vibaya na wamiliki wenye nia mbaya. Kwa mfano, kama ulivyosema, je, vikosi vya ulinzi vya Afrika vipo tayari kushughulikia tishio hili la kiusalama?

Elimu na Fikra Huru: Kwa upande wa elimu, ni kweli kwamba mashine zinaweza kusaidia lakini hazipaswi kuchukua nafasi ya uwezo wa kibinadamu wa kufikiri kwa kina na kubuni. Tunahitaji kuhimiza kizazi kipya kutumia teknolojia kama zana za kuboresha maisha, lakini si kama suluhisho la kila jambo.

Usalama wa Taarifa: Kuhusu vihifadhi data, jambo hili linaogopesha. Nchi nyingi za Afrika bado zinategemea teknolojia kutoka nje bila kuwa na uwezo wa kudhibiti habari na data zao. Hii inatuweka katika hatari kubwa ya kushambuliwa au kudhibitiwa kwa urahisi.

Mwisho wa yote, lazima tutumie akili bandia kwa hekima. Tuiangalie si kama tishio bali kama chombo cha kuboresha maisha yetu bila kuacha misingi ya utu wetu na thamani ya maisha. Maendeleo ya kiteknolojia ni muhimu, lakini yanapaswa kuwa na mipaka ili yasituondolee utambulisho wetu kama binadamu.

Ujumbe huu umejaa hekima kubwa, na ni wito kwa jamii yetu kufikiri kwa kina kabla ya kukumbatia teknolojia mpya bila mipango ya kujilinda na kuboresha ustawi wa watu wetu.
 
Mtu mwenye akili hajawahi kutesa au kunyanyasa wenzake hata siku moja. Isipokuwa labda hao watu wanaomiliki hizo AI waamue kufanya uharibifu. Lakini kama mashine ina akili haiwezi kufanya uharibifu hata kama imepewa amri na mmiliki wake.

Lakini pia katika Sehemu ambayo kuna akili bandia, huwa kuna watu wanaofanya kazi pale na kila mmoja ana ndugu zake wanaoishi uraiani. Kwahiyo haitakuwa rahisi mmiliki wa hizo Akili bandia kufanya umafia peke yake bila kuhitaji msaada kutoka kwa watu wengine. Na hao watu hawawezi kukubali wote kufanya hicho kitu
 
Why hiyo Gadget itumike kama inaleta hasara. Unalipwa kufanya kazi tu. Teknolojia mpya ikija jitahidi ujifunze kujua inafanyaje kazi na kuitumia vizuri, hapo haitakuReplace.
We would better completely abondon the use of technology, kama argument kuhusu teknoloji na za watu wanaoijua teknnoloji ndiyo hizi
 
Dunia inahitaji aina ya binadamu kama wewe, Uinuliwe Katika mawimbi ya juu Ili uishi kama taa kwa wengine
 
Ungefaa kuwa kampeni ya kitaifa maana Katika viwango sahihi vya maisha, "your business is my business " wanaopaswa kufanya maamuzi are silent....sisi tuendelee kusema
 
Your total wrong!!! But I do respect your opinion...

Wenye akili wanafanya biashara ya faida no matter inagharimu UHAI wa MTU, Fanya tafiti kwenye sekta zote nyeti.....UCHUMI,ulinzi ,afya,kilimo, elimu,dini....kote kupo corrupted
 
Dunia inahitaji aina ya binadamu kama wewe, Uinuliwe Katika mawimbi ya juu Ili uishi kama taa kwa wengine
Asante sana kwa maneno yako mazito na ya kutia moyo! πŸ’―πŸ™ Maneno kama haya yanazidi kunipa nguvu ya kuendelea kuwa msaada na mwanga kwa wengine. Naamini sote tuna nafasi ya kufanya dunia kuwa mahali pazuri zaidi kwa kushirikiana na kusaidiana. Ubarikiwe sana na uendelee kuwa na mwanga huo huo kwa watu wanaokuzunguka! 🌟
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…