AI (Artificial Intelligence) inaupeleka ulimwengu kwenye uharibifu mkuu, kwanini nawaza hivi?

Usiogope bado sana wangekuwa wanatuma maroboti yakapigane vita vijana wapumzike majumbani, pia kuhusu maswali kuwepo kwenye chtgpt ni kuwa Kuna ajira watu wa kila kabila na lugha wako wanafeed hizo mambo Kwa system lengo ni kupunguza kazi ya pepa work.
 
Your total wrong!!! But I do respect your opinion...

Wenye akili wanafanya biashara ya faida no matter inagharimu UHAI wa MTU, Fanya tafiti kwenye sekta zote nyeti.....UCHUMI,ulinzi ,afya,kilimo, elimu,dini....kote kupo corrupted
Mtu mwenye akili anawaza kusaidia wengine, sio kutesa wengine
 
Mada muhimu Kuna tatizo la ajira na robots zitaingia kazini je tatizo litakuaje?..tatizo tunaona ni mbali kumbe...
Kwanini tunafanya kazi ?
Na kama tunaweza kupata mahitaji tunayohitaji kwa wakati husika bila kufanya kazi unaona ni busara kuendelea kufanya hio kazi for the sake of doing it ?
 
Na iwe kheri kwetu sote
 
Kwani ikitokea kukawa na machine ambazo zinafanya Kila kitu, halafu binaadamu tukabakia kuendeleza tu maisha Kwa kuzaana Kwa wingi na kuijaza Dunia Kuna tatizo Gani? Hebu fikiria mtu hawazi atapata wapi kula, kuvaa, kulala na Kila hitajio muhimu Kwa ajili ya maisha yake, hizi njia ngumu za maisha ni sisi wenyewe tu tumejiwekea sijui sababu kubwa nini. Lakini naona ni kama zinaturejesha nyuma tu kufikia mafanikio makubwa, Kwa uzoefu uliopo mtu ambae anahangaishwa na tumbo lake hakuna Cha maana anaweza kukifanya kwenye hii Dunia, hebu fikiria mtu unafanya utafiti mkubwa was kuisaidia jamii lakini kula Yako mpaka uipiganie unadhani utafanikiwa? Kama ingelikuwa Iko ndani ya uwezo wangu ningebadilisha mfumo wa maisha huu tulionao Kwa Kila kitu, najua kwamba hii Dunia na vilivyomo kuvifikiria tu ni wazimu kabisa lakini sio watu wore ni wajinga kuwafanya wafikirie kula Yao na wasiwaze kitu chengine, na ndio maana Kwa kuzoea huu mfumo unaopotezea watu muda umewafanya watu wapoteze kabisa akili zao, labda ni Mimi tu akili yangu inawaza tofauti na haiogopi kuwaza visivyo wazika lakini naamini kama mtu hashughulishwi na tumbo lake, ana nafasi kubwa ya kufanya kitu Cha maana zaidi iwe Kwa ajili yake au Kwa jamii iliyomzunguka,Kwa mfano Mimi binafsi kama ingelikuwa sishughulishwi na tumbo langu basi naamini Dunia ingelikwisha kunitambua kama hapa duniani mungu kashusha kiumbe kinachoitwa Ahmed said na kafanya kitu Gani, lakini matokeo yake huu ugumu wa maisha unanifanya nisiwaze chochote zaidi ya kuhangaikia tumbo, sio kujiendeleza kielimu ya dini Wala kidunia, Kwa kweli mfumo huu wa kuchumia tumbo haufai kabisa, ni Bora tuache computer zifanye kazi na sisi tukibaki tukitumbua macho tu na kuangalia kinachofanyika na hiyo artificial intelligence. Kuna kitu hakipo SAWA katika hii Dunia na Kila mtu anajua lakini hakuna anaetaka kuchukua hatua, matokeo yake wenye akili kubwa wanaamua kutumia fursa na kuendelea kutuharibia maisha Kwa mifumo Yao ya ajabu, kitu kibaya zaidi hata wao hawafaidiki na chochote Kwa sababu na wao pia hawataishi milele, nawaza tu ikitokea Kuna mtu akavumbua kitu iwe ni chanjo au dawa itakayosababisha binaadamu kuishi milele asife, hivi unadhani viongozi wa dini na Dunia watamuacha salama? Wakati mfumo ushawaaminisha watu haiwezekani mtu kuishi milele? Itakuwa ni hasara kubwa kwao Kwasababu walifanikiwa kuwadanganya watu Kwa kipindi kirefu sana na hawakutegemea Hilo litikee, vyenginevyo huyo mtu atakaevumbua jambo Hilo awe na uwezo mkubwa sana iwe wa kimiujiza au kimungu wasiwaze kumfanya chochote bila ya hivyo lazima moto uwake, mpaka sasa naamini hii mifumo yetu tuliyonayo ya maisha ni kama gereza linalofanya tuweze kuona uhalisia. Utashangaa mtu anaposhindwa kumfanya jambo lake atamtupia mzigo wake mungu na kusema hili haliwezekani tusubirie miujiza ya mungu, utafikiri hiyo miujiza ya mungu nikitu ambacho Kiko mbali naye wakati miujiza mikubwa Iko mbele ya macho yake lakini anashindwa kuona Wala kuhisi, binaadamu mwenyewe ni miujiza mikubwa kuwepo kwake katika hii Dunia, hivi mtu anashindwa hata kufikiri maisha yake yalivyo anavyoishi, anavyotembea, anavyokula na Kila anachokifanya anaona ni kawaida sio miujiza? Bahati mbaya haya mambo yote yameelezwa mpaka kwenye vitabu vya dini lakini kutokana na huu mfumo wa kuhangaikia tumbo mtu anashindwa hata kujitambua yeye mwenyewe. Ni jambo la kusikitisha Kwa kweli lakini tumuimbe mungu atusaidie, maana mfumo umetubana hatufurukuti na tumeukubali Kwa nguvu zote, kiasi ambacho hatuhitaji kitu chengine chochote kitakachotusaidia kuuondoa huu mfumo wa kuchumia tumbo. Nawasilisha
 
Kwa tafsiri nyepesi ni mtu kuogopa kivuli chake mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…