AI inanifanya niwe na mashaka na umahiri wa wataalamu wetu wanaohitimu .

AI inanifanya niwe na mashaka na umahiri wa wataalamu wetu wanaohitimu .

Joined
Sep 22, 2026
Posts
64
Reaction score
124
Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza napata mashaka hivi hawa wataalamu wetu katika nyanja mbali mbali kama vile Afya, uhandisi ,ualimu na nyinginezo ,je ni kweli wanaohitimu Kwa uwezo binafsi au kupitia matumizi ya AI

Ukizingatia kwasasa vifaa vya kuibia kama vile simu ,miwani na nyenzo nyinginezo zenye access na Ai ambazo zinaweza kughishi majibu kwenye mitihani,na kazi za darasani

Hali inayorahisisha ufaulu bandia ,Kwa mfano Mwanafunzi anaweza kutumia AI kubashiri mtihani ,au akaingia na miwani Maalumu zenye uwezo wa kuscan mtihani na kutoa majibu

vile vile Ai zinatumika kwenye kufanya tafiti za kuhitimu kada mbalimbali kama vile afya tunaweza kuzalisha madakatri na wauguzi vilaza au kupelekea kuangukiwa na majumba kutokana na wahandisi wasio na umahiri na weledi .

Naomba nisieleweke kama napinga teknolojia hoja yangu ni kuwa kwasasa wanfunzi wengi wanaelekeza nguvu kubwa kusoma majibu badala ya maarifa husika kwenye vitabu mahususi
Kitu kinacho tishia usalama wa afya zetu, maisha na ubora wa elimu Kwa wanetu.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Back
Top Bottom