SI KWELI AI robot aonekana akifanya kazi shambani

SI KWELI AI robot aonekana akifanya kazi shambani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
<div class="bbWrapper"></div>
 
Tunachokijua
Maroboti ya Akili Mnemba (AI Robots/ Humanoid) ni kifaa kilichotengenezwa kwa kwa namna ya kuoneana kama binadamu. Baadhi ya Robots hutengenezwa na kupewa baadhi ya sifa zinazofanana na binadamu.

Builtin.com wanaeleza kuwa baadhi AI Robots/ Humanoid zilizozalishwa zimeleta athari chanya katika sekta mbalimbali ulimwenguni kama vile usafirishaji, utengenezaji viwandani nk. Hata hivyo matumizi yake sio makubwa sana duniani sababu ya gharama za juu za uendeshaji.

1721683360084-png.3049557
Tangu Julai 17, 2024 nchini Tanzania kumeibuka taharuki kwenye mitandao ya kijamii (hapa) kutokana na kuoneana kwa video inayomuonesha Roboti akiwa anafanya kazi mbalimbali za shambani. Jaombo hili limeshtusha watu ambao wamehitaji kujua ikiwa video hii ni halisi au la

1721683626891-png.3049560

Roboti akifanya kazi za Shambani

1721683659822-png.3049561

Roboti akifanya kazi za shambani
Ukweli ni upi?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa video hii ya roboti kufanya kazi za shambani haijachukuliwa katika mazingira halisi bali imetengenezwa kwa Akili Mnemba (AI). Zifuatazo ni baadhi ya sifa ambazo zimeisaiia JamiiCheck kuja na jibu hili:
1. Roboti anayeonekana kulima miguu yake ipo hewani (Hajagusa ardhi)

1721684400501-png.3049568

Miguu ya Roboti haijagusa ardhi​

2. Jembe linalima lakini Roboti anaonekana hata hajalishika

1721684457758-png.3049569

Roboti akionekana akifuatisha ishara ya kulima lakini jembe hajaligusa
3. Roboti akikata majani bila kuwa na kifaa cha kukatia

1721684939775-png.3049575

Roboti akioneana anavuna ngano kwa ishara ya kukata lakini hana kifaa mkononi
Hivyo, kutokana na sifa hizo JamiiCheck imejiridhisha kuwa video hiyo haikuchukuliwa katika mazingira halisi bali imetengenezwa kwa Akili Mnemba iliyomuingizia roboti na kufananisha matendo ya kilimo.

Je, wewe umeona nini zaidi?
Back
Top Bottom