- Source #1
- View Source #1
Nimeshangazwa na baadhi ya video ambayo inasambaa WhatsApp na group zingine ikionesha robot akiwa shambani analima kama mtu vile, saa nikajiulza hii ni edit au reality nakosa majibu.
Hivo nahitaji mniakikishie kwenye hilo maana kama ni kweli duuh watu watakosa kazi mbeleni for sure.
---
Video ya Roboti akiwa shambani
Hivo nahitaji mniakikishie kwenye hilo maana kama ni kweli duuh watu watakosa kazi mbeleni for sure.
---
Video ya Roboti akiwa shambani
- Tunachokijua
- Maroboti ya Akili Mnemba (AI Robots/ Humanoid) ni kifaa kilichotengenezwa kwa kwa namna ya kuoneana kama binadamu. Baadhi ya Robots hutengenezwa na kupewa baadhi ya sifa zinazofanana na binadamu.
Builtin.com wanaeleza kuwa baadhi AI Robots/ Humanoid zilizozalishwa zimeleta athari chanya katika sekta mbalimbali ulimwenguni kama vile usafirishaji, utengenezaji viwandani nk. Hata hivyo matumizi yake sio makubwa sana duniani sababu ya gharama za juu za uendeshaji.
Tangu Julai 17, 2024 nchini Tanzania kumeibuka taharuki kwenye mitandao ya kijamii (hapa) kutokana na kuoneana kwa video inayomuonesha Roboti akiwa anafanya kazi mbalimbali za shambani. Jaombo hili limeshtusha watu ambao wamehitaji kujua ikiwa video hii ni halisi au la
Ukweli ni upi?
Roboti akifanya kazi za Shambani
Roboti akifanya kazi za shambani
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa video hii ya roboti kufanya kazi za shambani haijachukuliwa katika mazingira halisi bali imetengenezwa kwa Akili Mnemba (AI). Zifuatazo ni baadhi ya sifa ambazo zimeisaiia JamiiCheck kuja na jibu hili:
1. Roboti anayeonekana kulima miguu yake ipo hewani (Hajagusa ardhi)
Miguu ya Roboti haijagusa ardhi
2. Jembe linalima lakini Roboti anaonekana hata hajalishika
3. Roboti akikata majani bila kuwa na kifaa cha kukatia
Roboti akionekana akifuatisha ishara ya kulima lakini jembe hajaligusa
Hivyo, kutokana na sifa hizo JamiiCheck imejiridhisha kuwa video hiyo haikuchukuliwa katika mazingira halisi bali imetengenezwa kwa Akili Mnemba iliyomuingizia roboti na kufananisha matendo ya kilimo.
Roboti akioneana anavuna ngano kwa ishara ya kukata lakini hana kifaa mkononi
Je, wewe umeona nini zaidi?