Tusipoyaandika au kuyapigia kelele vilivyo, mama aliye busy na kuifungua nchi atayasikia vipi na hasa kama wenye dhamana ni sehemu ya mchezo wenyewe?
Baada ya kuyasikia nilijivinjari kufika mpakani Rusumo kujiridhisha.
Huu ndiyo ulio ukweli mchungu:
Mgeni haingii nchini bila kutoa rushwa. Rushwa inaombwa waziwazi bila ya aibu. Rushwa imefanywa kuwa sehemu ya malipo halali ya waliopewa dhamana mbalimbali mpakani hapo.
Mambo ya aibu kubwa.
(Nitajivinjari mipaka mingine pia kuipata ladha kamili ya huko nako. Tutege masikio).
Mchezo uko hivi:
Mgeni akifika hupaswa kuanzia kitengo cha afya. Kuna mabwana na mabibi afya hapo. Cha mno huuliziwa kadi ya yellow fever.
Mgeni akiwa nayo hupewa ki memo cha kupeleka kwa afisa uhamiaji. Bila hiyo kadi, memo pia hupatikana kwa njia mbadala - pesa, wala si chanjo. Makubwa maana madogo yana nafuu!
Kihunzi hicho cha kwanza mgeni akikiruka, kwa afisa uhamiaji anaweza kuulizwa kuthibitisha kama kachanjwa korona.
Uhamiaji na korona wapi na wapi wandugu wakati kipo kitengo cha afya? Akikosa uthibitisho si kuwa atalazimika kuchanjwa, la hasha. Hapa napo chanjo mbadala ni pesa!
Mgeni akiruka viwili hivi mengi mengine yaja. Atatakiwa kueleza madhumuni ya safari, namba za simu za jamaa kama ana mwenyeji, jina la Hoteli atajayofikia kama hana mwenyeji, nk. Lini mla rushwa aliwahi kupungukiwa longolongo au visingizio?
Ole wake aseme kaja kufuata biashara. Makaratasi sasa yatakayotakiwa hapo kwa jina la leseni, vibali nk ili mradi mlengwa hawezi kutoboa. Kazi kweli kweli.
Au ole wake asijue jina la Hoteli au guest house atakayofikia, hapo napo ni kimbembe kingine cha kutosha! Bottom line kunatakiwa pesa na pesa lazima itoke.
Ama kweli kuna watu wako kwenye kulamba asali na kula kwa urefu wa kamba zao.
Ninakazia: Nani mwenye kuyaangazia haya, mama anapokuwa busy akiifungua nchi?
Pumzika kwa amani JPM yawezekana ulikuwa sahihi kuwa tutakukumbuka.