Aibu: Cosmas Cheka apigwa na Mmalawi lakini cha ajabu atangazwa kashinda

Aibu: Cosmas Cheka apigwa na Mmalawi lakini cha ajabu atangazwa kashinda

Hakika sijawahi kuona upendeleo kama huu kwenye mchezo huu wa ndondi popote, nimeangalia hili pambano nimeona aibu sana kwa matokeo ya uongo kama haya.

Kwa haya yanayofanyika, nchi hii haitoendelea kwenye michezo.
Me nishaachaga kufatilia mchezo huo kwa hapa nyumbani.
Mchezo wa ngumi, mtu akiwa kwao hapigwi!!!
 
Nilikuwa sijawahi muona Cosmas akipigana... Jana nimemuona...kiukweli uwezo wake ni mdogo sana...huwezi linganisha na alivyokuwa kaka yake enzi zile....yaani siku akikutana na bondia kama Mfaume....hakatizi hata raundi mbili.... bondia gani amelegea Kama binti...anarusha ngumi za kike kabisa eti ndio punch.... kujilinda hajui kabisa kila wakati yuko kwenye kamba.....kama anahitaji kuendelea na ngumi nashauri arudi gym kwanza....akatengeneze nguvu...hana nguvu kabisa...yaani kalegea....ndio maana watu wanashangaa utashindaje kwa ulegevu ule.
Miguu ka jogoo anapepesuka ovyo kabisa aibu tupu
 
Nilikua naangalia na mwanangu nikamfukuza mana niliona aibu dingi mzima kuangalia ngumi kama zile kazidiwa mtz mpaka noma alipgwa chuma kimoja down nikamwambia kesho shule kwenda kumbonji wakat gem zngne zote tunamaliza wote niliona aibu Mimi. Joke
 
Mi ngachoka hoi kwa ushindi wa Cosmas aibu aibu kabisa kinyaa. Mbinu za kiushindi za chama zimehamia kwenye uhalisia/majukwaa ya michezo, bora kura zinahesabiwa chumbani ila sio uamuzi uamuzi wa wale majaji.
 
Mvimbe mpasuke lakini haya yote ni mafanikio ya awamu hii, michezo inachana mbuga.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Refa mnamuonea Tu

Marefa wa. Mezani ndiyo wanaoweka point na kuzikusanya na kumtangaza mshindi

Anayesimamia pambano ni kama robot tu
 
Back
Top Bottom