AIBU: Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam walipeni wafanya usafi wa Soko la Ilala, hali ya soko ni mbaya

AIBU: Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam walipeni wafanya usafi wa Soko la Ilala, hali ya soko ni mbaya

ToniXrated

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
1,134
Reaction score
2,993
Habari zenu wakuu!

Siku ya jana nilifanikiwa kupita mitaa ya Soko la ILALA, jijini Dar-es -salaam,maarufu kwa uuzaji wa mbogamboga na matunda. Nilikuta hali ya usafi wa soko hilo ni mbaya kabisa kiasi kuhatarisha afya za wauzaji na wanunuzi wa bidhaa za matunda na mboga mboga. Yapata miezi mitatu toka Halmashauri ya jiji kuchukua majukumu ya ukusanyaji wa ushuru wa soko wa wafanyabiashara wa soko hilo ,mara baada ya mzabuni aliyepewa tenda ya kukusanya ushuru na kuhakikisha usafi wa mazingira ya soko kumaliza muda wake.

Yapata miezi miwili sasa wafanyakazi wanaofanya kazi ya kusafisha soko hilo kutokulipwa stahiki na mishahara yao. Hivyo kupelekea mgomo wa kusafisha mazingira ya soko hilo.Mbaya zaidi wale waliomstari wa mbele kwenda kudai mishahara na stahiki zao wameachishwa kazi.

Wafanyabiashara wa soko hilo kubwa katika nchi hii ya Tanzania, wamenijuza kuwa wamekuwa wakilipa ushuru wa shilingi 500 kila siku kwa halmashauri ya Jiji ila mpaka sasa hali ya soko ni chafu ni mbaya zaidi na kupelekea tishio la mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwa wakazi na wafanyabiashara wa eneo hilo.

Wito wangu kwa Halmashauri ya Jiji ni kuwa kama mmeshindwa kusafisha mazingira ya soko la Ilala licha ya wafanyabiashara kuwalipa ushuru wa mamilioni ya pesa kila siku, basi rudisheni tenda kwa mzabuni atakaehakikisha kuwa soko linakuwa safi muda wote.

Pia acheni uonevu kwa wafanyakazi wa usafi, wapeni haki zao wanazodai na acheni kuwatishia kuwafukuza kazi. Haiwezekani wafanye kazi miezi miwili bila ya malipo yoyote,mnategemea wakale wapi???

Cc:

Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam,Mh Amos Makala.

Mkuu wa wilaya ya Ilala

Meya wa jiji .
 
Idara ya mazingira na maliasil
Idara ya sanitation. Itakua ofisa wake yupo City Council environmental officer na kata inasemaje?
 
Hali ni mbaya sana,siku ya tatu leo soko halijafanyiwa usafi. Takataka kila kona
 
Halmashauri ya jiji tuondoleeni taka wakazi wa ilala

Hizi ni baadhi ya taka zilizolundikwa
 

Attachments

  • IMG_20221209_040313_5.jpg
    IMG_20221209_040313_5.jpg
    1.4 MB · Views: 9
  • IMG_20221209_040344_8.jpg
    IMG_20221209_040344_8.jpg
    1.7 MB · Views: 8
  • IMG_20221209_040333_1.jpg
    IMG_20221209_040333_1.jpg
    1.5 MB · Views: 8
  • IMG_20221209_040322_7.jpg
    IMG_20221209_040322_7.jpg
    1.5 MB · Views: 8
Back
Top Bottom