Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Nimeona picha za Mhe. Rais kuzindua Boti za Wavuvi huko Tanga.
Cha kusikitisha pamoja na nchi yetu kuzalisha Ma engineer tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mradi huo wa Boti za Uvuvi unazinduliwa kwenye Pwani ya Bahari ambayo haina hata eneo maalum la kisasa la kuegesha na kupaki boti hizo (Marina).
Cha kusikitisha zaidi pamoja na kuzalisha ma engineer hao miaka na miaka na kuwa na mamlaka za uvuvi na Bandari, bila kusahau vitengo vya PPP, Nchi yetu hatujawa bado na miradi ya ujenzi wa maeneo mazuri na nadhifu ya kupaki boti na meli kwenye bahari zetu na maziwa yetu ( Ukiondoa marina moja tu ambayo niliiona Masaki zinapopaki Boti za kukodi)
Rai yangu.
Naomba Ma engineer wa Tanzania na mliopo kwenye Mamlaka za Uvuvi na Bandari jitahidini sana kupata exposure nje ya nchi na kuja kuzifanyia kazi hapo nyumbani Tanzania. Ni aibu nchi yetu kuzindua mradi wa boti tena unazinduliwa na Rais alafu Boti hizo hazina eneo la kisasa za kuengeshwa!
Pia kupitia PPP waalikeni wawekezaji wenye uwezo watengeneze marina kwenye maeneo yetu ya maziwa na Bahari. Hili sio tu litafanya tuwe na fukwe nzuri ila linachochea uwekezaji na utalii katika uchumi wa bluu.
Kama hamuwezi ziambieni halmashauri zilizopo kwenye maeneo yenye maziwa na bahari kuwa na miradi ya namna hii maana hizi Marina zinaweza pia kutumika kama vyanzo vya mapato kupitia parking fee!
Kuweni na akili basi. Kama vipi tupeni kazi hiyo ya kuitengeneza na kuiboresha nchi yetu. Tena tutafanya bure bila kulipwa maana naona CCM wamewafanya mkose akili.
Mfano wa Maeneo maalum ya kisasa ya kuegesha Boti (Marinas) huu hapa 👇